MWANAMKE KUWA NA NYUMBA NDOGO(KIDUMU)......
tumezoea mara nyingi sana wanaume kuwa na nyumba ndogo ama wa pembeni kama watu wengine jinsi huviita, na hii mara nyingi imeonekana nikosa la mke ndilo humfanya mwanaume kutoka nje, lakini ni wakati wa fikra hii kubadilika kwani sio muda wote mwanamke humfanya mwanaume atoke nje, bali sasa mwanaume pia humfanya mke wake atoke nje....sababu za mwanaume kutoka nje wengi wamesema ni kwasababu ya uchafu, kutompa mapenzi akiwa anahitaji, ama kujibweteka, usipojipendezesha mwili na mengine mengi.. tumezoea sana kusikia hayo mpaka sasa yamekuwa sehemu za maisha yetu hamna la kushangaza hata kama leo usikie mume wako anamwanamke nje hushangai tena kwasababu atasingizia mambo mengi ambayo hata mengineyo siyo ya kweli wakati kumbe ni tamaa zake tu mwenyewe zimempeleka nje..
sasa basi wewe mume uliyeoa haitegemei unamiaka mingapi kwenye ndoa, jukumu lako kama mume unalijua ama unadhani kuweka chakula mezani na kuhudumia watoto ndio kila kitu, mwanaume kila siku urudi nyumbani kwako saa kumi za usiku mpaka majirani wanakusema wewe, mwanaume kutwa kumpiga mkeo hata kama kosa linastahili kumsema tu, mwanaume kumtukana mkeo mbele za majirani na marafiki unatukana mpaka sehemu iliyokuleta wewe duniani, unamvua nguo mkeo mbele za watu mwanaume matusi yanakutoka machafu kama gari la taka, mara mwanaume mpaka mama alie kukuomba penzi ndio umpe, looooohhhh inasikitisha...
unategemea huyo mke wako atakaa kukuvumilia kwa vituko vyako vyote kwa lipi, maana unapomtendea hayo mabaya kimbilio lake unalijuwa? ndipo nyumba ndogo huingia na hivi hawa nyumba ndogo wanavyojua kunyenyekea, anambembeleza mkeo kuliko hata wewe unavyoweza, anavyompa maraha, anavyomhudumia kaka hata siku moja husikii tusi likimtoka mdomoni sasa mke wako atabaki kukulilia wewe mpaka lini maana kila unapovumilia mwanaume bado anakuchokonoa kuna lengine la kufanya ama ni jukumu la mwanamke tu kuvumilia kwenye ndoa na sio mwanaume???????
hata kama kwenye biblia waliaandika mwanamke hujenga na kubomoa nyumba yake mwenyewe, utaibomoaje mwenyewe kwani unaishi peke yako kama shetani? tokea mwanzo Mungu aliumba Adam na Hawa inamaana kuna mwanaume atakayekufanya uibomoe ama kuitengeneza.. tusichukulie mstari huo wa biblia kama kisingizio wanaume mda wenu wa kujirekebisha ni sasa na sio kusingizia wake zenu..
sitetei nyumba ndogo lakini ni sisi wenyewe kama mke ama mume ndio huchangia, sasa baba kazi kwako, jitahidi kumchunguza mkeo ujuwe kama kwenye ndoa unamtendea haki ama la maana unavyozidi kumsogeza pembeni mwenzako wa pembeni anafurahia kusogezewa chakula kwa karibu na kujipakulia anavyotaka...
kazi kwenu waume....
0 comments: