Mwanamke maskini aliyefanyiwa miujiza..............Ni ajabu na kweli
Mwanamke mmoja
masikini sana alipiga simu katika kipindi kimoja maarufu kilichokuwa kikirushwa
na radio moja ya dini na kusema alikuwa anahitaji msaada ili apate chakula cha
familia yake kwa siku hiyo.
Tajiri mmoja
mwenye dharau na asiyependa kuona MUNGU akitukuzwa huku akiwa anasikiliza kile
kipindi akaamua afanye kitu kwa huyu mama.
Akainakili
anuani ya yule mama na kisha akampa secretary wake fedha na kuwatuma waende
sokoni na kununua vitu vingi pamoja na vyakula na fedha nyingi za kumpa yule
mama masikini na akasema akiwauliza nani kaleta nyie semeni mmetumwa na
shetani wa kibongo.
Baada ya
kununua na kubaki na fedha kama alivyoelekezwa na tajiri, yule secretary
akafika kwa yule mama na akashusha mizigo na kumpa zile fedha pia kama
alivyoambiwa.
Yule mama
akaipokea ile mizigo kwa furaha na kuwashukuru na kuanza kuingiza mizigo ile
ndani. Secretary akamuuliza yule mama, “Je ulitaka kujua nani katutuma tuilete
hii mizigo?”
Yule mama
akasema, “HAPANA, Haijalishi nani kaniletea mizigo hii baada ya kusikia
nikiomba kwa kupiga ile simu pale radioni, Maana MUNGU akiagiza hata shetani
hufanya kama MUNGU alivyoagiza”
Unajifunza nini
Mafanikio yako
ni kwa sababu ya uwepo wa nguvu za MUNGU, Hivyo Mungu daima atamalizia mipango
yako na kukupa mafanikio endapo utazidi kumcha yeye na kumshirikisha katika
kila kitu, haitajalisha ugumu wa jambo hilo kwa mungu kila kitu chawezekana.
Mungu atakupeleka mpaka juu ya kilele cha mafanikio na kukufungulia kitabu cha kumbukumbu ya mapito yako nasi tutajifunza kutoka kwa mafanikio yako.
0 comments: