Neno la leo
Zab 32:10 “Naye mtu mwovu ana mapigo mengi, Bali amtumainiye BWANA fadhili zitamzunguka”
TAFAKARI: Siku ya leo, mpe Mungu heshima, sifa, heshima, adhama kwa maana yeye anastahili vyote hivyo.Tumtumainiye Mungu katika maisha yetu siku zote, tukiwa kwenye raha ama shida.
SALA: Mwenyezi Mungu, asante kwa kunifanya mtu safi, Bwana najua sijakamilika katika njia zangu lakini wewe umekuwa ukiniangazia nuru ya uso wako siku zote.
Naomba usiniache Bwana kwa maana nakuhitaji zaidi katika maisha yangu. Naliinua jina lako na kulibariki kwa maana unastahili sifa. Katika jina la Yesu naomba na kupokea, Amen.
0 comments: