Nilihudumia mgomba kimiujiza bila kujua nikidhani namuuguza mme wangu

18:12:00 Unknown 0 Comments



Soma ina umuhimu sana na maisha yako

Binti mmoja aitwaye Antonia aliolewa na ndoa yake ikawa yenye furaha na mafanikio sana.

Antonia na mmewe wote walikuwa wafanya biashara waliokuwa wakikua kwa kasi nzuri.

Baada ya muda Antonia akaingiwa na tamaa ya kuwa na mafanikio zaidi ya mmewe ili apewe heshima.

Akasafiri na kwenda kwa mganga wa kienyeji na kuamua kujizindika na baade kurudi na kuendelea na kazi zake.

Wiki chache baadae mmewe akapata ugonjwa wa ajabu na kupooza mwili wake akawa ni mtu wa kubebwa, kuvalishwa, kulishwa kwa ufupi asiyejiweza tena.

Biashara zikaanza kudorora kwani Antonia alitumia muda mwingi kuzunguka na mmewe akisaka tiba na kuokoa uhai wake pia.

Akaanza kuwaza na kuona pengine ni ile dawa aliyoichukua kwa ajili ya kuizindika biashara yake. Akafunga safari na kwenda kwa mganga.

Kufika huko nusura azimie kwani mganga alikuwa kafariki. Ikambidi arudi na kuendelea kumuuguza mmewe kabla ya wazo kumjia na kuamua kwenda kanisani kwa maombi.

Maombi yakiwa yanaendelea mkanda wa ajabu ukafunguliwa kiunoni mwa mmewe na ghafla mme akaamka na kuanza kusimulia kuwa alikuwa kakaa kimazingira nje ya duka la mkewe akiita wateja.

Akasimulia pia kuwa alikuwa akirudi na kuona mkewe akiuuguza mgomba na kumwonea huruma na kulia ila akawa hana la kufanya.

Kuna mtu alikuwa akimjia na kusema nilitamani kukusaidia ila kwa kuwa nawe uliizindika biashara yako kishetani siwezi. Hivyo nikawa mtu wa kulia.

Baada ya hapo wote Antonia na mmewe wameokoka na wana furaha zaidi ya mwanzo..Na kila Antonia akikumbuka jinsi alivyotaka kuipoteza furaha ya familia kisa utajiri...huwa haishi kulia na kmwomba Mungu amsamehe.

Ndugu nami nakusihi hakuna njia yoyote ile ya mkato katika mafanikio itakayokujia bila ya majuto.

Inaweza kufanikiwa kwa muda mfupi ila mbeleni ina majuto makubwa na maumivu ya kutisha.

Eeh Mungu msaidie kijana huyu asomaye ujumbe huu apate mafanikio katika kila jema alifanyalo na uwe msaada wake katika mafanikio nasi tuyafurahie bila mtu kudhurika.

Comment AMEN kama waamini kila nafsi itaonja mafanikio hapa duniani kama inaamini uweza wa Mungu katika kutimiza malengo yake na sio nguvu nyingine.

Share na like Tabasamu na Fuledi na Wahenga Wapya

You Might Also Like

0 comments: