Nina miaka 25. Ni mzuri wa sura, Umbo na hata muonekano wangu wote. Napenda niolewe na mtu mwenye utajiri wa zaidi ya bilioni moja.

15:50:00 Unknown 0 Comments

Binti mmoja ambaye bado ni kinda na mwenye uzuri wa kupindukia siku moja aliandika kwenye mtandao mmoja maneno haya: 

************************************************
Subject: Nifanyaje ili niweze olewa na mtu tajiri? 

Naomba niandike ukweli wangu hapa: 

Nina miaka 25. Ni mzuri wa sura, Umbo na hata muonekano wangu wote. Napenda niolewe na mtu mwenye utajiri wa zaidi ya bilioni moja. 

Mnaweza fikiri labda nina tamaa za kimaisha lakini kwa Maisha ya hapa Arusha mtoto wa kike ambaye unataka kuishi Maisha ya kufurahi yasiyo ya taabu mtu mweye utajiri wa milioni 10 hana ubavu huo.

Mahitaji yangu sio makubwa sana.

Je kuna yoyote katika mtandao huu anayeweza kuwa na utajiri niutakao? Au wote mmeoa? Nitafanyaje ili niolewe na mme tajiri?

kwani katika wanaume nilio wahi kutembea nao wengi wana utajiri wa milioni 50n kushuka, jambo linaloonyesha kwa mahitaji yangu wataweza tetereka na biashara zao.

Hebu fikiri mfano tuamue kujenga nyumba yenye mahitaji ya muhimu ya familia, kwa mitaji hiyo nitawaharibia biashara zao kabisa kwani Arusha Maisha yako juu.

Hivyo naomba niulize maswali yafuatayo ya kunisaidia mimi:

1) Wapi watu matajiri wanapendelea kwenda kujirusha? (tafadhali niorodheshee sehemu mfano,bar, hotel na gym)

2) Niangalie zaidi matajiri wa umri gani?

3) Kwa nini wake wa matajiri wengi wanamuonekano wa kawaida? Kwani nimekutana na baadhi ya mabinti wenye muonekano wa kawaida lakini wameolewa na matajiri wakubwa pindukia.

4) Utajuaje tajiri huyu anafaa kuwa mmeo na anahelakiasi gani

Asanteni

Miss. Pretty aka Mtoto Mzuri
*********************************************

Mmoa wa waliongalia post ile alikuwa ni fuledi CEO wa tabasamu na fuledi nae akawa wa kwanza kumjibu:

***********************************************
Mpendwa Miss Pretty aka Mtoto mzuri,

Nimeisoma post yako nikiwa na hamu kubwa ya kuwa nawe na namini kuna wanawake wengi wenye matarajio kama yako.

Tafadhali naomba nieleze hali halisi nikiwa kama mtaalamu mwekezaji.

Nipo Arusha na nina utajiri wa zaidi ya bilioni 10 na ninaendana na mahitaji yako kupitia post yako, hivyo naamini sipotezi muda kukuandikia haya na kwa kila anayesoma.

Nikiwa kama mfanyabiashara,ni jambo la hasara kuchukua uamuzi wa kukuoa wewe.Na majibu yake ni marahisi sana.

Unachotaka kukifanya ni kubadilishana kativya “UZURI” na “HELA”:Ambapo Mtu A anatoa uzuri na mtu B anatoa fedha kama biashara ya kubadilishana.

Ingawa kuna tatizo kubwa katika uzuri wako,Uzuri wako utapotea na fedha zangu hazitapotea labda kuwe na tatizo la usimamizi.

Ukweli ni kwamba fedha zangu zinaweza ongezeka kila mwaka na wewe uzuri ukapukutika kila mwaka.

Kwa upande wa uchumi, mimi ni mali inayoweza kuthaminika,na wewe ni mali chakavu.

Kwamba baada ya miaka kumi uzuri wako hautakuwa kama wa sasa kutokana na umri kwenda na changamoto nyinginezo, ila hela yangu nikiisimamia baada ya miaka kumi naweza kuwa na zaidi ya utajiri huu.

Lakini nikichukua mfano wa biashara za mtaani, ni kwamba kitu kikishuka thamani unaweza kukiuza kwa bei ya chini na kisiposhuka ni faida kwako.

Sasa mimi utajiri ukishuka wewe utahitaji kumtafuta mtu mwingine wakati kama mtu angeoa mtu ampendaye hata utajiri ukishuka watabaki wote kwa furaha.

Mtu yoyote mwenye utajiri wa bilioni moja na zaidi sio mjinga atakachokifanya ni kulala na wewe kisha kukuacha bila masuala ya ndoa kwani kuwa na wewe ni hasara.

Kwa wewe kuja kuwa tajiri mwenye utajiri wa bilioni moja ni rahisi kuliko kuja kumpata tajiri mwenye utajiri wa bilioni na akawa mjinga wa kukuoa wewe.

Naamini majibu haya yatakufaa

Imesainiwa,
Tbasamu na Fuledi CEO

Funzo

Wanwake ni bora kujituma kufanya kazi na kuweza kujitengemea kuliko kukaa ukisubiri kuwinda matajiri wenye hela waje kuwa waume zenu

Wanaume tunatakiwa kuwa makini sio kila binti mzuri wa sura anayekufuata wakati umefanikiwa ana mapenzi ya dhati wengine kwao ni ajira

You Might Also Like

0 comments: