Nyumba yabomoka michepuko yanusurika

19:13:00 Unknown 0 Comments

Kulikuwa na nyumba moja iliyojengwa karibu na uchochoro mmoja ambao ilipitiwa na watu wengi.

Uchochoro ulitumika na watu wa aina tofauti na wenye uelewa tofauti kila mmoja akiwahi zake katika mishunghuliko yake ya maisha.

Siku moja alipita kijana mmoja mwanahabari  ambaye aliichunguza sana ile nyumba na kugundua kuna ufa mkubwa katika ile nyumba.

Akauangalia kwa makini ufa ule na kuupiga picha akiona hatari yake mbeleni na kisha akaandika habari pamoja na picha zile  akitadharisha kuwa ,

" kama watu wasipohamishwa katika jengo hilo basi kuna uwezekano wa watu kupoteza maisha yao"

Habari ile ikasambaa kwenye magazeti, radio, TV na mitandao ya kijamii na hatimaye wiki chache baadae serikali ikawahamisha watu  na nyumba ile ilianguka siku chache baadae kutokana na ufa ule.

Ninachotaka hapa kukukumbusha ni kwamba bila kutumia jicho la tatu katika kutafakari mambo yatuzungukayo kamwe hatuwezi pata mafanikio au kujitoa katika hali ngumu zituzungukazo.

Jioni njema

You Might Also Like

0 comments: