Silii kwa kasababu ya bili kuwa kubwa hapana, ila nalia kwa kuwa Mungu alinifanya nikojoe kwa miaka 70 bila kulipa bili .................

13:06:00 Unknown 0 Comments

Mzee mmoja alifikia miaka 70 na akakumbwa na ugonjwa uliomfanya ashindwe kukojoa vyema.

Daktari akamwambia kuwa atatakiwa kufanyiwa upasuaji mdogo ili aweze kupona vizuri.

Mzee akakubali kwa kuwa alikuwa akipitia maumivu makali sana kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa huo kila akojoapo.

Baada ya upasuaji mzee akaonyesha kuendelea vyema na wakati anatoka daktari akampa bili iliyohusisha malipo yote aliyokuwa akidaiwa.

Mzee baada ya kuichukua ile bili akaiangalia na kisha akaanza kulia kwa uchungu sana na kila mtu pale akaamumia.

Baada ya kuona hali ile daktari akamuuliza kwa nini unalia? Kama bili ni kubwa basi tunaweza kukufanyia utaratibu wa kulipa kidogo kigo.

Mzee kajibu, “ Silii kwa kasababu ya bili kuwa kubwa hapana, ila nalia kwa kuwa Mungu alinifanya nikojoe kwa miaka 70 bila kulipa bili .

Lakini leo ili niweze kukojoa vyema imenibidi nilipe bili…… Nilisahau kabisa kumshukuru Mungu kwa miaka yote hii 70 kwa kunipa upendeleo huu”

Je nawe msomaji umekumbuka kumshukuru Mungu wako kwa kila kitu alichokupa bure bila malipo ?


penda Tabasamu na Fuledi

You Might Also Like

0 comments: