Story mbaya kuliko zote..admin bado analia
Pichani mtoto huyu na wadogo zake maisha yao
yalikuwa ni ya raha sana wakati wazazi wao
walipokuwa hai, Baba mfanya biashara na Mama
Mwalimu...
Matatizo yalianza pale wazazi wote walipofariki
katika ajali ya gari iliyotokea Mbeya ambapo gari
ilitumbukia katika mlima nyoka na wazazi wake
kufariki pamoja na wadogo zake wawili na kubaki
yeye na dada yake wa kwanza ambaye nae
alikuwa kidato cha pili..
Baada ya hapo, mali za marehemu baba yake
zilitaifishwa na Benki kwani baba yake alikopa
Benk na nyingine marafiki wa baba katika
biashara kugombania hivyo kuwachia nguo tu na
mali kidogo ambazo ndugu wa baba yake
walizigawana.
Mirathi ya mama yao ilitoka lakini shangazi zake
walidai kuwa madogo hawana chao, hivyo
wakaachwa juu juu na wao wakaamua kwenda
dar kusaka maisha.
Dada yeye akawa house girl na dogo akawa
akizunguka mtaani kusaka riziki.
Kwa sasa dogo anataabika hana pa kulala wala
kula na hana msaada wowote na dada yake
kashanyiwa mikasa ya ajabu na sasa hajulikani
alipo..
Nyie ndugu msio na roho za huruma acheni tabia
hizo kwani Mungu anaona mnayoyafanya...!!
Mkiwa makanisani mnajifanya kutoa sana sadaka
kumcha Mungu lakini nyuma yenu mnafanya
mambo ya ajabu ya kugombania mali za
marehemu na kuwacha vijana wanasota mtaani
bila huruma na wakati wazazi wapo mlijifanya
kina anko safi
MUNGU ANAWAONA ACHENI HIZO MAMBO
0 comments: