Taabia za watu hutokana na sisi tunavyowafanyia wao..
Kuna siku moja mzee mmoja mwenye hekima na busara zake alikuwa amekaa sehemu ya kupumzikia pale kijijini kwake.
Msafiri mmoja akaja na kumuuliza swali, "Ni watu wa aina gani wanaoishi katika kijiji hiki, kwa sababu nahitaji kuhamia hapa kutoka kijijini kwangu?"
Yule mzee mwenye hekima naye akamuuliza swali, "Ni watu wa aina gani waliko katika kijiji unachotaka kukihama?"
Msafiri akajibu, "Hawana mbele wa nyuma, wakatili , matapeli, wezi, wapenda rushwa, usikope kidogo watakudai kwa kukushikia panga yaani kwa kifupi sio watu wa kuishi nao kabisa."
Mzee mwenye hekima akamjibu, "Na kijiji hiki kuna watu wa aina hiyo hiyo pia hivyo karibu sana."
Baada ya muda kidogo msafiri mwingine akaja na kuuliza swali lile lile kwa yule mzee, mzee naye akamuliza, "Ni watu wa aina gani walioko katika kijiji chako?"
Yule msafiri akajibu, "Wanakijiji ni waelewa sana, wakarimu, wapole na ni wazuri kuishi nao kiukweli nitawakumbuka sana."
Mzee mwenye hekima akamjibu, "Hata hapa watu wanishi hivyo hivyo."
Funzo ni lipi hapa?
Kiuhalisia tunaiona dunia na watu waishivyo sio kama ilivyo, ila kama sisi tulivyo.
Mara nyingi taabia za watu hutokana na sisi tunavyowafanyia wao..
Maisha ni mafupi sana kwa sisi kutopendana… Tuishi kwa furaha.
0 comments: