Usiiamimi habari hii ni uongo wa kuianza week mpya
Mke wangu pamoja na kuhisi kuwa naweza kuwa na mahusiano na mabinti wengine lakini hakufanikiwa kupata ushaihidi wowote ule kwani nilimzidi ujanja.
Kama ningekuwa siku hiyo na mchepuko basi ningejaribu kutengeneza majukumu na hata kujifanya nawahi kurudi nyumbani halafu jamaa yangu angenipigia simu kuwa nahitajika kuondoka hivyo wife asigundue kitu.
Na mwiko wangu ulikuwa kulala nje ya nyumba kwani huo niliuona kama utumwa wa mapenzi so nikawa na mega kisela kwa timing.
Ijumaa moja jioni nilimwambia mke wangu kuwa nitachelewa kidogo kwani tuna part ya kuagana na mfanyakazi mwenzetu pale ofisini kwetu hivyo nitarudi saa sita au saba kasoro lakini nilikuwa namdanganya kwani nilikuwa na miadi
Siku hiyo nilitakiwa kukutana na mtoto mmoja aitwaye mariam ambaye kwanza tulifahamiana naye hapa facebook na pamoja na kuwa na marafiki zaidi ya 4000 ila kidume nilimpa sera za maana na hatimaye akawa wangu.
Mara ya kwanza nilionana naye .mitaa ya soweto mbeya baada ya mimi kuchanganyikiwa na picha zake za facebook na instagram ambapo nikam-ad fb na kuendelea kuchati naye huku simu mpaka laptop yangu ikawa na picha zake japo siku isipite bila kumcheki.
Siku hiyo soweto hatukukaa sana akawa yuko busy ila macho yangu yaliridhika sana na kumwona binti mariam na nzuri zaidi ni lile busu alilonipiga pale shavuni basi kila dakika nilijikuta nasisimuka ama kweli ile siku sitaisahau.
Ijumaa hii nilikuwa tayari nimewahi kutoka zangu ofisini nikiwa na rafiki yangu suphiani tumekaa sehemu tunapata moja baridi na moja moto huku.nikiendelea kuchati na mtoto kupitia whatsapp akiniambia anakaribia maeneo tuliyopo na usalama wa nyumbani ukiwa saafi kwani alijua wife anajua nipo kwenye part.
Mariam aliingia pale akiwa na rafiki yake na meza yetu ikagawika kwa wanaume wawili na kina dada wawili ambao kwa pamoja walikuwa sasa wakila maisha na kuonekana wana furaha sana.
Pombe ziliendelea huku tukifurahia maongezi mpaka pale rafiki yangu aliponikonyeza tuhame kiwanja na kwenda sehemu tutafute hotel yenye vyumba ili mengineyo yakikaribia kusiwe na shida.
Tukaondoka mpaka hotel moja iliyojificha nje ya mji na kuendeleza vinywaji huku vyumba vikitungojea ili tufanye yetu mpaka mida ya saa sita na madakika ili baada ya hapo tuwahi wajumbani.
Baada ya kutwika pombe za kutosha nikaingia chumbani na baada ya kazi nzito tukajipumzisha kitandani.
Nakuja kushtuka ni saa kumi na mbili kasoro ya asubuhi na kina sms zaidi ya 20, missed calls zaidi ya 50 kutoka kwa mke wangu na baadhi ya marafiki.
Kuangalia kitandani mariam hayupo na kukagua baadhi ya vitu vyangu naona vipo, ile kushusha mguu chini naona damu kwenye kitambaa chake.
Nikaingia bafuni nakumwona kaanguka chini na hajiwezi akihena kwa shiida, nikamnyanyua na kumweka kitandani kisha nikagonga chumba cha rafiki yangu na kugundua hayupo na gari langu halipo.
Kuuliza reception naambiwa walikuja watu watatu wakamgongea mlango na kuondoka naye majira ya saa kumi alfajiri.
Nilichokifanya nikamchukua mariam na kuita tax mpaka hospital na kupewa huduma ya kwanza na nashukuru hakuchukua saa fahamu zikaja na kumbe huwa ana tatizo la kupoteza fahamu na kutokwa damu hivyo akaendelea na matibabu nami nikaondoka nikijifanya naenda kuchukua fedha.
Muda huo ni saa mbili na nusu asubuhi kila nikimpigia rafiki yangu hapokei simu na kichwa kikiwa kimechanganyikiwa na gari na wakati huo huo mke wangu akinipigia simu na nikawa sipokei.
Nikiwa nimesimama pale mara yule rafiki akatokea na gari kumbe muda ule alimpeleka yule binti aliyelala nae baada ya kudai kuondoka na wale watu walionekana nao walikuwa wakija kuwachukua wateja wengine.
Baada ya kujadili pale jambo la haraka ikawa ni kwa mimi kujifanya nilishikwa nikiwa naendesha gari kwa kasi huku nimelewa hivyo niko kituo cha polisi na aliyetakiwa kumpigia mke wangu ni rafiki yangu ili aje na mke wangu wanilipie fedha kituoni baada ya mimi kuongea na rafiki yangu mmoja ambaye ni askari.
Nikaenda kituoni na saa moja baadae akaja mke na kunilipia nikiwa natokea mahabusu kisha tukaondoka na kuelekea nyumbani kumbe lilikuwa deal.
Nikaenda nyumbani na masaa mawili baadae nikaenda hospitali kumlipia bill mariam na kisha nikamrudisha kwake.
Hakika ilikuwa ni siku ya majanga ambayo kamwe sitaisahau milele.
Usiiamimi habari hii ni uongo wa kuianza week mpya
0 comments: