Wewe ungekuwa dan au salome ungefanyaje?
Salome yeye anafurahi kuwa na mme mtulivu asiyependa anasa kama pombe na wanawake.
Mara nyingi dan ambaye ni mme wa salome yeye akitoka kazini hurudi nyumbani kumsaidia kazi mkewe na hata akitoka basi huenda kuchaza mpira wa kikapu na kurudi na mra moja moja husindikizwa na mkewe.
Baad ya muda mrefu Dan na Salome wakaamua kwenda club ili wakumbushie enzi zao.
Wakaondoka mpaka club na walipofika mlangoni mlinzi akamwambia Dan karibu kaka naona siku mbili tatu umetususa.
Salome akauliza yule ni nani, dan akadai ni mlinzi wa kazini kwao hulinda na hapo nyakati za usiku kuongeza kipato na salome akaelewa.
Wakafika ndani club na kwenda moja kwa moja sehemu ya vinywaji. Bar maid akaja na konyagi na kumfungulia dan na kuuliza huyu atakunywa nini?
Dan akajibu atakunywa bavaria bar maid aakaenda kaunta wakati salome anajiandaa kuuliza dan kaanza kunywa lini bar maid akawa karudi na kusema nimewaandalia chumba namba 112 tangulieni nawaletea vinywaji
Salome akapaniki na kuanza kukimbia kwenda nje na kupanda tax hata kabla hajamwambia dereva endesha dan akaingiaa.
Wakati huo salome analia kilio cha chini, dereva akamuuliza dan vipi leo naona hamjaelewana poa na huyu malaya maana analia na alitaka kukimbia au anaogopa mambo yako yale ya saudia.
0 comments: