HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " SEASON 3

14:55:00 Unknown 0 Comments



HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

 SEASON 3

Soma mwendelezo wake


ILE TEXT ILIANDIKWA HIVI, " Unajifanya mjanja?? utaona" kwa kweli nilishtuka sana, moyo wangu ukaanza kwenda kasi kiasi cha kwamba nilihisi muda wowote naweza nikapoteza fahamu..

Nilijiuliza mambo mengi sana kichwani mwangu hivi nipo ndontoni au nipo katika ulimwengu wa kweli?. Fahamu zilipokuja kunirudia nikajikuta karibu na mlango wa nyumbani kwangu.

Ghafla nikasikia sauti kutoka kwa mke wangu ikiniuliza, " Mbona umesimama muda mrefu sana hapo ukiwaza, kuna nini?"  Nikajibaraguza kwa kucheka na kumshika mkono na kumvuta karibu na mpaka wa eneo la nyumba yetu.

Nikamwambia, "Unajua nini mke wangu? majirani zetu wote nyumba zao zina mageti, kasoro sisi tu. hili suala linanisumbua sana akili yangu, hasa nikiwaza kuhusu ulininzi.

Unakumbuka kazi niliyoenda kufanya kule Iwindi? Pesa nitakazopata kule nitaweka ukuta na geti haya bwale wanaokumbendea mendea niwakomeshe........ Tukacheka na kushikana mikono na kuingia ndani lakini kichwani mwangu nkitafakari kuhusu ile meseji.... " Unajifanya mjanja?? utaona"

Asubuhi yake nikiwa ofisini nikakumbuka kuwa nilitakiwa kujibu email za ofisi hivyo nikaiwasha laptop yangu na kuanza kuzipitia emails kwenye akaunti yangu.Moja kati ya email niliyokutana nayo wakati nasoma ilinipa mshutko mkubwa sana kiasi cha kwamba sikuweza kuendelea kuzisoma zile email nyingine.

Tumbo la kuhara likanibana na nikakimbia haraka kwenda chooni na kurudi haraka. Mhudumu wa ofisi akanitani kaka mbona leo shuzi zako kali hivyo? sikumjibu nikajifanya kutabasamu na kuingia ofisini kwangu nakuanza kuisoma ile email vizuri.

Email ile iliandikwa hivi "washa simu yako nakutafuta" nilizidi kuchanganyikiwa kwani hadi nafika ofisini kwangu simu yangu ilikuwa nimeiwasha,sasa nikajiuliza maswali mengi sana simu yangu imejizimazimaje na muda gani ilijizima wakati ilikuwa na full charge?

Pia huyu aliyenitumia email ni nani?na nilipojaribu kureply ile email ilikataa,na nilipo rudi kuiangalia tena ili nisome imetoka kwa nani,cha kushangaza na cha kuogopesha zaidi ile email ilikuwa imejifuta,kwa kweli kijasho chembamba kilinitoka ingawa ndani ya ofisi kulikuwa na AC.

Sasa nikaamua kuiwasha simu huku nikitetemeka kabla sijakaa sawa simu ya ofisi ya mezani ikaita kwa sauti ya juu sana nikaruka kidogo safari hii nigongeshe tako langu kwenye ukingo wa meza.

Sikutaka kuipokea nikamwita haraka mhudumu na kumwambia aipokee, alipoipokea wealiongea dakika kama tatu kisha akanipatia na yeye kutoka nje.

Sauti niliyoisikia ilikuwa ya yule dada ambaye mara kwa mara tumekuwa tukiwasiliana naye bila kumjua jina lake. Akasema, sapraiiiz hata nimeku-miss nikaona nikupigie simu nikusalimu sina mengi nitakutafuta usiku kwenye simu yako ya mkononi kuna kitu nyeti nataka tujadili......... hakuongea zaidi akakata simu.

Niliishiwa nguvu na kuanguka chini...................................................................................................................................(nilipoanguka chini nini kiliendelea?........................... 

Itaendelea kesho kama itapata mdhamini mpya asante kwa Edna Tracy, Simon Condrad, Nyandison Morali , Kalmas Konzo na Rose Mushi

Unaweza kudhamini mwendelezo wa kisa hiki cha kusisimua kwa shiling 2000 tu kupitia 0713317171, 0762436068, 0684868191 pia kama una swali juu ya kisa hiki nicheki kupitia whatsapp 0713317171

Bofya hapa kusoma hadithi hii ilikoanzia

You Might Also Like

0 comments: