HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 4

15:29:00 Unknown 0 Comments

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

Season 4

ILIPOISHIA JANA

Sauti niliyoisikia ilikuwa ya yule dada ambaye mara kwa mara tumekuwa tukiwasiliana naye bila kumjua jina lake. Akasema, sapraiiiz hata nimeku-miss nikaona nikupigie simu nikusalimu sina mengi nitakutafuta usiku kwenye simu yako ya mkononi kuna kitu nyeti nataka tujadili......... hakuongea zaidi akakata simu.

Niliishiwa nguvu na kuanguka chini.............................................................

Soma mwendelezo wake

BAADA ya kuzinduka nikajikuta nipo hospitali nikiwa nimezungukwa na ndugu na marafiki. Sikuamini nilichokiona nikafikiri nipo ndotoni.

Mke  wangu akanihoji, " nini kilikukuta mme wangu? Maana nilipigiwa simu kuwa umeanguka ghafla na umeletwa hospitali na pia vipimo vinaonyesha ulipatwa na mshtuko mme wangu, Ni mshtuko gani mme wangu?"

Ingawa nilikuwa nimeshaanza kupata nguvu, kutokana na lile swali nikajifanya sina hata nguvu ya kulijibu swali maana ingenipa mshtuko wa pili hata kabla ya kutoa maelezo yake. Jioni yake nikaruhusiwa kutoka na kurejea nyumbani.

Zilipita takribani wiki tano nikiwa nimeirushia chooni ile laini tena choo cha shimo ili nisiweze kuiona tena.

Hata kama nipatwa na wasi wasi baada ya kukumbuka enzi za udogo wetu tuliwahi mchukia paka wetu kisha tukamshika na kumtupa katika choo cha shimo ili asiwe taabu tena kwa kunya kitandani na kwenye unga.

Lakini maajabu yake baada ya kumtupa na kuridhika kuwa yuko shimoni muda wa chakula alikuja akiwa na kinyesi yaani wote tuliduwaa na kunifanya kuwachukia kabisa paka.

Lakini kwa hili niliamini kuwa ni suluhu na hata yule mhudumu wa ofisi nimwambia asipokee siku yoyote ya kunitaka mimi private zaidi ya kuwambia wanitafute bila kuwapa namba yangu na zile za kiofisi ajibu.

Nilichukua likizo ya wiki mbili pale ofisini na kumwambia mke wangu twende nje ya mji tukapumzike na nikatumia mwanya huu kumkumbusha kuwa nilitakiwa kufanya hivyo kwa ushauri wa daktari hasa baada ya lile la shinikizo kuwa nilizidisha kazi mno.

Niliondoka na familia yangu kwenda matema nje kidogo na mji wa Mbeya  huku nikiamini sasa lile tatizo limeisha.

Kweli zilipita siku tatu nikiwa pale kwa furaha na familia yangu nikiwa na marafiki wapya na simu nyingi nilizopigiwa zilikuwa ni za ndugu jamaa na marafiki.

Ijuma mmoja usiku wa saa nne nikiwa nacheza na mwanangu huku napata mvinyo wangu mara simu ikaita kuangalia ilikuwa ni namba ngeni.

Nilipotaka kupokea tu ikakata na kwa kuwa sikuwa na muda wa maongezi na ilikuwa ni usiku nikaachana nayo.

Jumapili usiku nikiwa na mke wangu tumelala pale hotelini, simu ilipigwa tena na wakati huu iliita sana na mtu wa kwanza kuisikia alikuwa mke wangu.

Akaichukua simu na kunipatia, si wajua tena hawa ndugu zetu walivyo aleji na simu wakijua ni michepuko.

Basi mimi nikaichukua ile simu na kuipokea kwa loudspeaker nikijiamini kuwa sina mchepuko.Ila kwa bahati mbaya mpigaji alisikika hewani ila hakuongea neno nikakata simu na kulala.

Jumatatu mchana nikiwa nimekaa pembezone mwa ziwa napunga upepo nilipokea sms iliyosema "Nitakupigia usiku" kutoka kwenye namba ile ile ya jana yake usiku.

Nikataka kupata uhakika wa kuwa ni nani huyo ambaye hawezi kuongea mchana mpaka usiku. Nikaupiga ile namba ila haikupokelewa basi sikuitilia maanani.

Nikaendea kupunga upepo pale na si wajua tena mandhari ya matema ilivyoyakuvutia? Zilipita dakika 20 nikapokea sms kutoka katika namba ile ile ikisema, " wee endelea kupunga upepo tu, nimeshakuambia nitakupigia. Huelewi nini hapo?"

Nilinyanyuka haraka na kuelekea usawa wa ziwa bila kujua naelekea wapi? Mara ghafla nikashtishwa ba sauti ya mwanangu akisema baba na mimi nije kuogelea?

Ile nageuka tu nilichokiona...................................... Fuatilia kisa hiki kesho mida kama hii

NAKUTAKIA WEEKEND NJEMA

You Might Also Like

0 comments: