Kamwe usizidharau nguvu zako chache zinazopotea ukiwa wafanya jambo fulani huwezi jua zinawabariki wangapi

00:42:00 Unknown 0 Comments

Kijana Dan asiye na elimu alipata kazi na kuajiriwa katika jumba moja la kifahari na kazi yake kuu ikawa ni kuchota maji kutoka mtoni na kuyajaza katika pipa moja kubwa.

Alipewa madebe mawili na kila siku aliyatumia kuchotea maji na kutumia mti na kamba kuyaweka begani ili aweze kuyabeba kwa wakati mmoja.

Debe moja lilitoboka na kila siku alivyokuwa akitoka na maji mtoni yalipungua na kufika na debe moja likiwa nusu na lile moja likiwa limejaa kabisa.

Dan alichota maji yale kwa muda wa miaka miwili kila siku akitumia yale madebe mawili na moja likiwa limetoboka na kufika na maji yakiwa nusu ingawa alijaza pipa baada ya kwenda mtoni mara nyingi.

Baaada ya miaka miwili kazi ile ikawa imefikia mwisho kama makubaliano na dan akaonyesha kuumia sana na kumwambia mwajiri wake amsamehe kwa kuwa debe moja lilitoboka na kushindwa kufikisha maji yote na laiti maji yale yote yangefika si ajabu angeyafanyia kazi nyingine nyingi.

Mwajari wake akamwangalia na kumbwambia, " Dan!!! Kwani hujagundua katika kipindi hicho chote njia ya kutoka kisimani imepandwa maua mazuri na yakuvutia?,  "

Dan akajibu ndio nimeyaona

"Baada ya kugundua debe lilimetoboka na linamwaga maji basi mimi nikapanda maua na kila ulivyotoka mtoni uliyamwagilia na mke wangu amekuwa akiyachuma na kuyapamba ndani mwetu, Bila wewe na debe hilo tusingepata wazo la kuyapanda maua hayo.... asante sana na haya ni malipo yako"  akampa cheki ya fedha nyingi kijana dan

Funzo

Kamwe usizidharau nguvu zako chache zinazopotea ukiwa wafanya jambo fulani huwezi jua zinawabariki wangapi

Na pia usijilinganishe na wenzako wenye uwezo mkubwa kama lile debe kubwa huwezi kujua wewe kidogo chako kinaweza kuleta mambo gani mazuri kama lile debe dogo lilivyoweza kufanya kazi nzuri kwa kusaidia maji kujaa kwenye pipa huku likimwagilia maua....Tambua wapi udhifu wako unaweza kugeuka na kuwa fursa 

Tangaza kupitia blog hii wasiliana whatsapp 0713317171

You Might Also Like

0 comments: