Karuka mkojo kakanyaga nani hiii.... binti huyu kaniboa kabisa....hebu nawe msome... yaani bogaz sana
Chichi alizaliwa katika familia ya kifukara iliyokuwa ikiishi kijijini kwao kilolo iringa kabla ya kuhamia jijini mbeya ambako baba yake mzazi alihamia huko baada ya kupata tenda ya kujenga nyumba ya kampuni ya Tabasamu na Fuledi.
Pamoja na ufukara wa familia ya mzee chichi ila vijanaume vyenye uchu wa kuparamia kila binti walishagundua kuwa chichi ni almasi iliyofunikwa na vumbi mchangani.
Yaani ilitakiwa kumgharimu mtu kuichukua almasi hiyo kuipa maji ili iwe na mng'aro wa kutosha na hatimaye kuingizwa katika ulimwengu wa kuthaminishwa na kuwatoa jasho wanunuzi.
Akabahatika kumaliza form six kwa shida kabla ya kwenda chuo kilichopo jijini mbeya ambako kwa mara ya kwanza jamii kubwa ya watu wenye hela zao wakaanza kumwona akiwa zaidi ya mlimbwende wa kawaida.
Ni katika kipindi hiki ambako kijana mmoja maarufu jijini mbeya mwenye utajiri wa kutosha aitwaye Yuzo na ambaye anamiliki migodi ya madini huko chunya na zaidi ya visima nane vya mafuta nyanda za juu kusini na baadhi ya utajiri usio endana na umri wake alipoamua kutumia jeuri ya pesa kuhakikisha anampata mtoto chichi.
Kwa ufupi chichi hakujaliwa upole na utulivu tuu bali pia umbo lake na mpangilio wa mavazi yake na hata tabasamu lake kwa wakati huo lingeweza kukufanya usiwe na kiburi cha kutomsifia.
Kama haitoshi yangeweza kukupata yaliyonipata mimi baada ya kumtazama kwa muda na kusahau nipo barabarani na kufanya bodaboda yangu inipe kovu la kudumu ambalo ilibidi niliite hilo kovu "chikovu" kovu lililosababishwa na chichi.
Yuzo hakuwa mtu wa kuongea zaidi ya kutumia mapambe ingawa juhudi hizo ziligonga mwamba kwani Chichi alibaki na msimamo wa kuwa na kijana mmoja ambaye yeye alifahamiana nae tangu sekondari na kwa wakati huo walikuwa wakisoma pamoja.
Kijana huyu yeye alikuwa ni handsome na kila mwanamke angependa kuwa na kijana wa aina hii ili aweze kutoka nae kwenye mialiko mingi na kuwaumiza wenzake.
Kama ujuavyo wanawake wa sasa lazima wawe na wanaume watatu, mwanaume mwenye pesa za kumhudumia binti na binti hapa anakuwa hana upendo wa dhati kwake zaidi ya pesa.
Wa pili ni mwanaume mweye mvuto ambaye huyu atapenda kuongozana nae katika kila mitoko ili kuwarusha roho marafiki zake.
Na watatu ni mwanaume wa kuoa huyu anatakiwa kusubiri mpaka binti aaamue kuolewa, na huyu huwa haonekani sana zaidi ya watu wa chache kumfahamu na wengi mtakuja kumfahamu wakati wa mahari au sendoff tu.
Hivyo chichi alibaki na msimamo wake na kuwa na huyu kijana wake handsome ingawa ushawishi wa yuzo ukazidi pale alipomwita chichi na kumwomba akaunti na baada ya kupewa yeye akamwekea kiasi cha shilingi milioni mia moja zilizompa wazimu chichi.
Wakati chichi akiwa katika ndoto hiyo ambayo kwa sasa ilikuwa ikielekea kuwa ya kweli zikawa zimesalia siku nne kabla ya birthday yake.
Siku ya birth day watu wakaja wa kutosha na yuzo akaalikwa pia na yule mpenzi wa chichi alikuwepo na wakati wa zawadi yuzo akakabidhi chichi funguo za gari jipya la kifahari aina ya bentely.
Ni zawadi hii ikamfanya chichi na yule mpenzi wake wakae na kuteta kuwa chichi ataenda kukaa na yuzo amlie hela ili waje wawe na miradi yao na kuoana hapo baadae.
Yuzo akampangishia nyumba nzuri na ya kifahari chichi maeneo forest mpya jijini mbeya na kumlipia pango la zaidi ya dola 500 kwa mwezi ikiwa na kila kitu ndani na chichi yeye akaingia na nguo zake alizozivaa tu.
Akaanza kuishi pale na yuzo alimpenda sana na baaada ya miezi kadhaa kusonga maisha ya chichi yakawa ni mazuri kupindukia na yuzo akamshirikisha mpango wake wa kufunga harusi ili wawe mke na mme wa kihalali.
Lakini maneno ya chini kwa chini yakaanza kumfikia yuzo kutoka kwa mashushushu wake kuwa chichi bado ana mahusiano na kijana yule handaome pamoja na kuonywa mara kadhaa na yuzo.
Tabia hiyo ikakithiri na mara hii yuzo hakuvumilia tena na kumfukuza chichi ikiwa ni pamoja na kumnyang'anya kila alichompa na chichi kufanikiwa kuondoka na kiasi kidogo cha fedha na duka moja la siri alilokuwa akilimiki mitaa ya kabwe.
Akaondoka na kuanza kuishi na yule kijana wake na kuendeleza bishara zao na wakati huo mme alikuwa akifanya biashara ya kuuza laptops na simu.
Haikupita muda mrefu baadae wakafunga harusi na kuanza kuishi kama mtu na mme wake.
Mwaka mmoja baadae chichi akabahatika kupata mtoto wa kike na maisha yakazidi kwenda mbele.
Zikaanza kusikia habari mtaani kuwa mme wa chichi sio riziki
lakini chichi akapuuzia kwani siku hizi kijana akiwa na maendeleo kidogo na ni handsome basi watu
hawataacha kumpa kashfa kibao na hasa ukizingatia kazi za mishemishe nazo huwa na
majanga yake.
Hata chichi alipoulizwa kuwa kwa nini mmewe anakuwa karibu sana na baadhi ya watu wenye sifa mbaya ambao wanatokea uarabuni alipuuza kwani alimwamini sana mme wake.
Na pia alijiuliza mbona deal zake nyingi ni dubai na oman kwa
hiyo ni kawaida tu ukizingatia huko ndio kuna watu wa rangi hiyo.
Kuna siku chichi akamuomba
ruhusa mmewe aende kijijini kwao akawasalimie wazazi na bila hiyana mme akamwekea gari tayari pamoja na vijisenti vya kuwapa wazazi na kuwa chichi angekaa
kule kwa muda wa wiki mbili.
Kwa bahati mbaya hakuweza kukaa siku zote kwani kuna tatizo lilijitokeza ikambidi arudi
mapema bila kumwambia akijua wangejadiliana kunako nyumbani akifika salama.
Chichi hakuamini kwani kufika nyumbani tena kwenye chumba chao cha kulala akaiona boxer ngeni isiyoendana na ya mme wake na baada kumuuliza ni ya nani?
Mme akanijibu kuwa ni ya shamba boy, akajaribu tena kuuliza
ilifikaje ndani kwo? akadai usiku alikuwa anaogopa hivyo akawa akilala na shamba boy.
Ulikuwa ni mtihani kwa chichi hasa ukizingatia maneno yale ya mtaani lakini ilimbidi aamini huku akijiuliza kama baba anakuwa
muoga sasa wana famialia wanaohitaji ulinzi wake
itakuwa vipi?
Basi yakaisha na maisha
yakaendelea. Ilipita miezi na sasa ni mwaka ambapo wiki iliyopita amemfumania live mmewe akiwa na jibaba la kiarabu tena bila aibu juu ya kitanda chao cha ndoa wakifanya mambo ya ajabu kuandika.
Chichi alishtuka na kidogo azirai lakini alijikaza hasa ukizingatia hakutaka majirani wapate hili, kwa
aibu mmewe akamfuata na kumwambia amsamehe kwani
ni mara ya kwanza na amefanya hivyo ili apate deal la kwenda Dubai kufanya shoping ya
nyumba na ofisi yao mpya.
Kweli chichi ameamua kumuachia nyumba na ameondoka na mtoto na mpaka sasa amepanga sehemu ambapo ameanza maisha
mapya na anasema kamwe hata onana na mmewe huyu wala kumruhusu mtoto wao aonane na baba yake maana ni laana.
Chichi kila akimfikiria yule tajiri yuzo haachi kulia kwani anaona ni bora angebakia na yule.....
Hadithi hii ni ya uongo
Siku njema
0 comments: