TAHADHARI : MATUMIZI YA SIMU YAKO NA USALAMA WAKO

04:42:00 Unknown 0 Comments





Bwana Juma ni Dereva Taxi maeneo ya Mwanyamala kwa kopa siku moja alifuatwa na jamaa mmoja ampeleke Sinza kwenye nyumba fulani ya kufikia wageni .Walipofika pale Yule jamaa akasema ameishiwa chaji kwenye simu yake hivyo akamuomba Juma simu yake atumie kupiga ili awasiliane na mwenyeji wake pale nyumba ya wageni hata hivyo simu ya Juma haikuwa na hela.

Walipokaribia ile nyumba ya wageni Yule jamaa akaomba kushuka anunue vocha atie kwenye simu ya juma halafu awasiliane na mwenyeji wake, Juma akakubali. Jamaa akanunua vocha akaingiza kwenye simu ya Juma kisha akawasiliana na mwenyeji wake.

Walipofika sehemu husika jamaa akashuka akaingia ndani ya nyumba kumfata mwenyeji wake ambaye alikuwa mwanamke huku Juma akiwa ameshaondoka zake kwa sababu alikuwa ameshakamilisha shuguli yake.

Siku iliyofuata iligundulika maiti ya mwanamke ndani ya kile chumba cha nyumba wa kufikia wageni, ambapo simu ilikuwa mezani na vitu vingine vyote. HAli yam le chumbani haikuonyesha kama kulikuwa na vurugu au mikiki yoyote ile.

Uchunguzi wa awali ulifanyika pale chumbani ikiwa ni pamoja na kwenye kifaa cha kuwekea taka na simu ya Yule mwanamke aliyekufa, na pia mwili wake ukapelekwa chumba cha maiti ukifanyiwa uchunguzi zaidi.

Kwenye kifaa cha kuwekea taka iligundulika vocha moja iliyotumika, ilipofuatiliwa iligundulika iliwekwa kwenye simu ya Juma ambayo ilitumiwa kumpigia huyu mwanamke aliyekutwa na mauti. Dereva wa taxi, Bwana Juma, akatafutwa akapatikana, na ukaguzi ulipofanyika kwenye gari lake ikagundulika vocha nyingine ya simu iliyotumika katika moja ya milango ya taxi hiyo.

Hivi sasa Bwana Juma yuko mahabusu ambapo anashikilwa kwa mashtaka ya mauaji na uchunguzi unaendelea kufanyika mpaka hapo itakapokuja kujiridhisha si yeye aliyefanya tukio hilo.

Inawezekana wewe ukawa ni Bwana Juma ajaye, unayependa kugawa simu yako tu kwa watu wapige, watu waingize vocha zao, watu waandike ujumbe mfupi au wafanyie chochote kile bila kufahamu kuwa unachofanya kinaweza kuhatarisha maisha ya wengine na yako pia.

SIMU NA NAMBA YAKO NI MALI YAKO IMESAJILIWA KWA JINA LAKO, WAKATI UNASAJILI ULIINGIA MKATABA WA KUTUMIA KIFAA HICHO BILA KUVUNJA SHERIA ZOZOTE ZA NCHI MUDA WOTE.

Kina Juma wako wengi, tazama na chukua tahadhari usiwe mmoja wao .

Mtumie rafiki yako au umpendae nami nimetumiwa na rafiki anayenijali

You Might Also Like

0 comments: