KUOMBA MSAMAHA PALE MNAPO KOSEANA NI JAMBO BORA PIA
Barua kwa rafiki,
Tulipo hitilafiana na kuamua kuishi kama maadui nilifikiri lilikuwa jambo la kishujaa na nikaona niishi peke yangu bila ya kuwa nawe rafiki tuliyeishi na kushirikiana kwa miaka mingi.
Najua kweli kosa lilikuwa lako, laini kutokana na funzo ulilonipa naamini sasa mie ndio mkosaji mkuu na pengine sikuwa na busara kutofuata hatua ulizozifuata wewe.
Kitendo cha kuniomba msamaana na kunisihi tuyasahau na kuwa tena ndugu wapya, ulikuwa uamuzi wenye busara na ujasiri mkubwa sana. Najuta kwa nini pengine mimi sikuwahi kuja na kukuomba msamaha kwako rafiki.
Ni kweli watu wengi tumekuwa na tabia za kuamini ya kuwa kuombana msamaha pale mnapo kosana ni kujifedhehesha na kushushiana heshima, lakini ni jambo ambalo kila mtu anatakiwa kuwa wa kwanza kulitetea na kuhakikisha urafiki unazidi kudumu.
Umenipa funzo na katika hili namini sitakuja kukosana nawe na katika maisha haya nitajitahidi kuwa mwepesi sana kuimarisha mahusiano yangu na jamaa zangu kuliko kutumia dakika moja kusambaratisha mahusiano yaliyo dumu kwa miaka mingi.
Bila wewe ningejifunza somo hili,
Asante
Fuledi

0 comments: