MAMBO MACHACHE YA KUYAJUA KUHUSU SIKU YA JUMATATU!
1. ASILIMIA 50 YA WAFANYAKAZI HUCHELEWA KAZINI.
(Wengi huwa hawaamini kwamba Jumatatu imefika na wanatakiwa waende kazini)
2. TAKRIBANI DAKIKA 10 ZA KULALAMIKA.
(Watu wengi hutumia zaidi ya dakika 10 kulalamika pindi waamkapo siku ya Jumatatu)
3. WATU WENYE UMRI MKUBWA HUUMIZWA ZAIDI NA SIKU HII.
(Wenye zaidi ya miaka 40 huwa wanapata shida sana na hutumia muda mwingi kulalamika pindi ifikapo Jumatatu)
4. UZALISHAJI NA UFANYAJI WA KAZI HUWA CHINI YA ASILIMIA 30.
(Wafanyakazi wengi huweza kufanya kazi kwa umakini kwa masaa 3 ama chini ya hayo)
5. NI SIKU INAYOONGOZA KWA WATU KUJIUA.
(Kutokana na makala iliyoandikwa kwenye BBC News miaka ya nyuma, kasi ya watu kujiua ni kubwa siku ya Jumatatu kuliko siku nyinginezo.Mfano 16% ya wanaume na 17% ya wanawake wamejiua siku hii ukilinganisha na 13% ya waliojiua siku nyinginezo)
6.HUONGOZA KWA WATU KUPATA MASHAMBULIO YA MOYO (HEART ATTACK)
(Kutokana na British Medical Journal 20% ya ongezeko la mshambulizi ya moyo yametokea siku ya Jumatatu kutokana na msongo wa mawazo na shinikizo la damu)
7. INASEMEKANA NI SIKU YENYE MVUA KIDOGO KULIKO SIKU NYINGINEZO ZA WIKI!
8. NI SIKU NZURI YA UNUNUZI WA MAGARI.
(Wauzaji wengi wa magari huwa hawategemei wateja kununua gari siku ya Jumatatu, kwahiyo ukienda kununua unaweza pewa punguzo kubwa la bei.)
0 comments: