Ticha: Neno gani linaanza na herufi K na linaishia na herufi A ambalo huleta raha

10:59:00 Unknown 0 Comments

(Joni) dogo wa darasa la
kwanza kafika shule
akaanza kulalamika kwa
mwalimu wake wa darasa
kwamba la kwanza si saizi
yake na anataka arushwe hadi darasa la tatu kwa
maana anaamini ana akili
kumzidi hata dada yake
ambaye yuko darasa la
tatu. Ticha wa darasa
kuona dogo kazidi kupiga kelele na kusumbua
akamchukua akaenda naye
kwa mwalimu mkuu. Ticha
wa darasa: Huyu mtoto
hata simuelewi, darasani
anapiga kelele kwamba anataka apelekwe na
darasa la tatu kwamba la
kwanza si saizi ya akili zake. Ticha mkuu akapigwa:
Ngoja nimuulize maswali ya
la tatu akishindwa arudi
darasani na akae atulie
vinginevyo acheze na
bakora. We mtoto, tatu mara tatu ngapi?
Joni: Tisa mwalimu.
Ticha mkuu: Tisa mara 4?
Joni: 36
Basi ticha mkuu
akamkandamiza dogo maswali kibao ya darasa la
tatu dogo akawa anapatia.
Ticha mkuu: mwalimu mi
naona kijana yuko sawa,
hebu mpeleke tu darasa la
tatu, fanyeni utaratibu wa kumuingiza kwenye
atendensi ya darasa la tatu.
Ticha wa darasa: sawa
mwalimu ila ngoja nimuulize
maswali zaidi. Joni ni kitu
gani ambacho ng'ombe anavyo vinne na mimi
ninavyo viwili?
Joni: Miguu
Ticha: Kitu gani unacho
ndani ya kaptula yako ya
shule ambacho mimi sina? (Ticha mkuu akashtuka
kuhusu hilo swali)
Joni: Mifuko
Ticha: Kitu gani mbwa
anakifanya halafu
binadamu anakikanyaga? Joni: Kujisaidia haja kubwa
njiani. (ticha mkuu mdomo
ukawa uko wazi
anashangaa)
Ticha: Kitu gani ukikiingiza
ndani kinakuwa kigumu na cha rangi kama nyekundu
au pink lakini kikitoka
kinakuwa kilaini na
kinanata nata? (Ticha mkuu
jicho likamtoka lakini kabla
hajamzuia dogo kujibu dogo akatoa jibu)
Joni: Big G.
Ticha: Kitu gani mwanaume
anakifanya akiwa
amesimama, mwanamke
akiwa amekaa na mbwa akiwa kasimama kwa
miguu mitatu?
Joni: Kujisaidia haja ndogo. Ticha mkuu akaanza
kutetemeka. Ticha: Neno gani linaanza na
herufi K na linaishia na
herufi A ambalo huleta raha
sana watu wakilitamka? Joni: KULA Ticha mkuu akavuta pumzi
ndefu halafu akazishusha
akasema: Mwalimu naona
mpeleke Joni darasa la tano.
Maswali yote sita ya
mwisho mimi mwenyewe nimekosea majibu yake.

You Might Also Like

0 comments: