Mbaya sana.... usisome

08:05:00 Unknown 0 Comments

Salome akiwa na umri wa miaka 17 alikutana na kijana mmoja ambaye alimrubuni na kufanikiwa kumpata na miezi michache baadae salome alijikuta akikimbiwa baada ya kuwa mjamzito na jukumu la kumlea mtoto kuwa lake.

Akafanikiwa kurudi shuleni baada ya kujifungua na kumtunza mtoto wake na masomo yakaendelea kwa ufanisi na kufanikiwa kuhitimu vyema mafunzo ya sekondari.

Akiwa chuoni mwaka wa pili akakutana na kijana ambaye alimshawishi mapaka akafuta lile wazo lake la kuwachukia wanaume baada ya Dan kumwambia kuwa angemwoa pamoja na kuwa ana mtoto.

Dan akaendelea mbele na kumvisha pete ya uchumba na wakati huo salome akiwa na mimba ya miezi miwili ya dan. Dan alifurahia sana mahusiano hayo kabla ya kumtoroka miezi saba baada ya salome kujifungua na kuoana na halima.

wakati huu salome aliwekwa chini ya uangalizi wa karibu na baadhi ya ndugu baada ya kuokolewa katika majaribio matatu ya kutaka kujiua na moja likiwa la kuitoa ile mimba.

Mida ikapita na mtoto akawa mkubwa na wakati huu akawa kabahatika kupata kazi katika shirika moja la kijamii lenye kuwasaidia walemavu pale mkoani kwake na maisha yakwa mazuri.

Kazi zikaenda vyema na maishaq yakasonga mbele na akasahau kila mkasa wa maisha yake na kuzidi kumshukuru mungu ampe mafanikio na uvumilivu wa kuwatunza wanae wawili.

Mwaka wa nne akiwa pale akizini akajikuta akiwa katika mapenzi mazito na romeo ambae yeye baada ya kusikia mkasa mzima wa maisha ya salome akaahidi kumtunza na kumfanya aweze kuyasahau hayo yote na kufurahia mapenzi mazito.

Walidumu kwa mwaka mmoja na nusu wakiwa na furaha kabla ya mke wa romeo kuja na kuwafumania na kumwacha salome akiwa  na jeraha kubwa la nyembe usoni mwake.

Salome wakati huu alikuwa na mimba ya romeo ambayo pamoja na jitihada za kuitoa mwisho wa sku akajifungua mtoto wa tatu. Ilimuuma sana na kila wakati sasa akaanza kuwaangalia wale watoto kwa masikitiko na kuona kama alikuwa na mkosi au bahati mbaya katika maisha yake.

Kuwa na watoto wa tatu wa baba tofauti na kila baba na majnga yake kulimfanya salome kuwa katika msongo wa mawazo usio na tiba na kuna nyakati tofauti aliripotiwa kuonekana akiwa mpole tofauti na zamani na ule uso wa tabasamu kugeuka na kuwa wenye mikunjo ya hasira.

Siku moja baada ya kuwaza kwa siku kadhaa bila majibu na ikiwa ni mwisho wa mwezi mshahara wake umetoka, aliwachukuwa wanae na kwenda hoteli moja ya kifahari sana na kupanga chumba cha ghorofa ya 10.

Alikula chakula kizuri na wanae na baada ya kuhakikisha wanae wamefurahi vya kutosha, usiku ule akaandika urithi wake kwa wanae na kuamini kuwa siku ya pili yake ingekuwa siku ya mwisho kwa yeye kufurahi na wanae.

 Alifanya hivyo kwani usiku wa pili yake angejirusha kutoka katika dirisha la chumba hicho kilichopo ghorofa la 10 ili ajiue na kuhitimisha maisha yake ambayo yamekuwa ya kuumizwa hapa duniani huku hata nduguze wakigeukia na kumwona mwanamke malaya asiye na hadhi ya kuishi katika jamii ile.

Asubuhi siku ya pili aliamka akiwa hana jambo la kufanya zaidi ya kuwa na chupa yake ya wine na glass ndogo iliyokuwa na wine kiasi cha kawaida akinywa huku akiangalia watoto wake wakiamka wakila na wakicheza.

Watoto wake walionyesha furaha na kuwa hakuwa na wazo lolote lile kichwani mwao zaidi ya kuwa na furaha. Alijiulza maswali mengi na kukosa majibu kwa nini wao walikuwa na furaha vile na akamua kuwauliza.

Walipoulizwa wote walijibu walifurahi kwa kuwa mama yupo na wanafikiri maisha ni mazuri tu, akajiuliza kwa nini yeye hana furaha na yuko pale muda huo. Na je kujiua ni suluhu ya matatizo? Salome alisitisha kujiua na kurudi kuendelea kuishi na watoto kwa furaha na amani na mpaka sasa amefanikiwa kuwakuza na kuwa na msimamo na wanae akiwaepusha kunaswa katika njia alizozipitia yeye.

* Maisha sio kuangalia ni mara ngapi umekosea ila angalia katika kila kosa ni nini kilibakia hata kwa chembe ndogo kikakupa fajara kisha endelea na maisha








You Might Also Like

0 comments: