MGANGA WA JADI AUA MGONJWA WAKE KWA KUMTANDIKA FIMBO NA KITU KIZITO KICHWANI WAKATI AKIMTIBU NYUMBANI KWAKE

09:47:00 Unknown 0 Comments

Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Vicent Kawawa(28) ameuawa kwa
kupigwa na fimbo na kitu kizito
kichwani na mganga wa kienyeji
aliyekuwa anamtibu ugonjwa wa akili nyumbani kwake katika kijiji cha
Buduba kata ya Nyandekwa wilayani
Kahama mkoani Shinyanga.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa
Shinyanga SACP Justus Kamugisha
alisema tukio hilo limetokea Agosti 5
mwaka huu saa 12 jioni.

Alisema Vicent Kawawa(28) mkazi wa kijiji cha Buduba akiwa nyumbani kwa mganga wa jadi aitwaye Mihayo Isheli akitibiwa ugonjwa wa akili aliuawa kwa kupigwa na fimbo na kitu kizito
kichwani na mganga huyo na watu
waliokuwepo eneo la tukio na
kusababisha kifo chake papo hapo.

Kamanda Kamugisha alisema chanzo cha tukio hilo ni kwamba mgonjwa alipandisha kichaa na kuanza kumpiga mganga wa jadi na watu waliokuwa eneo hilona ndipo katika kumtuliza mganga alianza kumpiga akisaidiwa na watu hao
ambao idadi yao haijajulikani na
kusababisha kifo chake papo hapo.

Alisema baada ya tukio hilo mganga
Mihayo Isheli alikimbia na familia yake pamoja na watu waliokuwa katika eneo hilo na kamba jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi sambamba na kumtafuta mganga huyo wahusika wengine waliokuwa katika eneo la tukio.

Chanzo:Bongo Leaks

You Might Also Like

0 comments: