Nanenane jinsi ilivyonipa mpenzi bomba
Mara yangu ya kwanza kuonana na binti huyu iliwa ni tarehe 8 ya mwezi wa nane au maarufu kama siku ya nanenane nkiwa natembelea mabanda ya maonesho ya wakulima.
Nilishtuka na kuduwaaa nikimtazama kwa dakika kama mbili kabla ya mpenzi wangu niliyekuwa nimeambatana naye kuniganyaka kwa ishara ya kuonesha hasira na wivu baada ya kuhisi namkodolea sana mimacho huyo dada.
Nikatoa macho na kujifanya kama na msoglea zaidi yule dada na kuinama kuchukua kipeperushi kimoja cha banda hilo pembeni ya yule dada jambo lililomfanya mpenzi wangu tulipotoka nje anombe samahani kwani alifikiri mimi namtolea macho yule dada kumbe mimi niliangalia zaidi kipeperushi kile.
Nikajifanya nami kuonesha kuumia na kumwambia siwezi kumwangalia binti yoyote wakati na wewe nupo hapa Darling......... lakini ukweli ni kwamba sina uhakika kile kipeperushi kiliandikwa nini.
KWanza niliumia kwakuwa sikupata bahati ya kuchukua namba zake ili niwasialiane naeye na pili ni wapi nitamwona tena nikashikwa na hasira na kuichukia siku ile yaani sana sana na kwa hasira nikakitupa kile kipeperushi.
Tukazunguka hapa na pale na kisha nikawa nimechoka na ,mpenzi wangu yeye akaingia kwenye kibanda cha Gracia Cosmas ili anunue keki nami nikawa nimekaa kwenye kibanda fulani nikiwa na napata soda kali.
Kuna katoto kadogo kakaja na kusema kaka samahani kipeperushi hiki ulikitupa shangazi kasema nikupe. Ahhhhh nikachukia zaidi maana nikahisi atakuwa mnoko mmoja kaniona nimetupa kile kikaratasi sasa yeye ni myangizi mle ndani sasa nanikomesha.
Nikakichukua na kukiweka kwenye mkoba wangu pale mezani na punde tukawa tunaondoka kuelekea nyumbani. Tukiwa njiani kwa kuwa mamaa alikuwa akiendesha gari mimi nikaona kupoteza muda nisome kile kipeperushi.
Ebwana nyuma yake kukawa na namba ya simu na ameandika niadd whatsapp mara moja.Mmmh niakjifanya sijaona ili mama asishtuke na kuisave ile namba na kukitupa kile kipeperushi nje na nikamtafuta yule mwenye namba.
Kidogo nicheke kwa sauti lakini nikajikaza kumbe ilikuwa namba ya yule binti maana picha ya profile ilikuwa yake. Nikasema kimoyomoyo hawa ndio watoto wajanja wanaotakiwa katika dunia ya leo sio mtu anajua unampenda naye hafanyi juhudi za kujisogeza huyu ndio.
Nikamtumia meseji
Mimi:"Hola" akajibu
Yeye: Hello Mzima wewe?
Mimi: Niko poa asante kwa namba,
Yeye: Usijali sana, umenichekesha sana pale ulivyoweza kujifanya ulikuwa huniangalii na kuokota kile kipeperushi
Mimi: ha ha ha ha ha LOL (hata kama sikujua maana yake mie nikaiweka tu)
Yeye: Nikaona unajikanyaga kutaka kuomba namba au kunifahamu nikatumia trick ya kumpa mtoto namba akuletee
Mimi: Wewe ni kiboko na jasiri sijawahi ona... truly nimekupa salute.
yeye: Karibu
Mimi: Unafanya nini hapa mbeya? Ni sura ngeni?
Yeye: Nafanya na TNB Blog,
Mimi: mmh siwapati ndio nani hao?
Yeye: Fuledi Blog ............
Mimi: ooooh namfahamu sana huyo , kwani paoja na uchizi wa zile ndoto zake ana ofisi?
Yeye: Yaap mie ni marketing manager pale si waona kuna matangazo mle so mie nashugulikia hilo na pale nane nane tulikuwa nabanda letu...... nawe unakaribishwa kuleta tangazo.
(Nikaona niutumie mwanya huo kujifanya nataka kutangaza bila hata kuwa na duka wala chochote cha kutangaza)
Mimi: Ok so nina biashara yangu kutangaza pale kwa mwezi au mwaka bei gani?
Yeye: Laki tatu tu kwa mwezi na mwaka tunajadili na pia inategemeana na biashara bei inashuka au kupanda na kwa jinsi unavyolipia muda mrefu bei pia inapungua.
Mimi: Okey Okey so i will send you down payment of 150, 000 na kesho jioni tuonane ili niweze malizia na kukupa tangazo langu la mwezi
Yeye: WOw!! asante sana ....... CIAO
Unaambiwa kwa takribani miaka kama sita hivi sina uhakika kama kuna siku niliwahi kurufahi kama siku hiyo nikawa najiimbia imbia kwenye gari mpaka mamaa akaniuliza kunani mbona furaha imeibuka ghafla?
Nikamdanganya kuwa nimelipwa hela angu hulani hivyo nitakutoa out leo jioni, naye akafurahia na kisha tukaongoza mpaka nyumbani na jioni tukatoka.
Siku ya pili mida ya jioni mtoto akaiendea hewani nami nikamwambia hotel ya kuonana na dakika chache baadae tukawa pamoja. Mtot kiukweli ameumbika na huwa watu kama hawa sipendi kuelezea maana hata wewe unayesoma kwa jinsi ulivyo na wivu utaweza nionea wivu au kumwazia mabaya mtoto wangu... muone kwanza unavyoona aibu... kazi umbea tu kutaka kujua mambo ya watu.
haya tuachane na hilo basi kifupi mtoto ni mrefu ambaye kifuani ni kama ana miaka 18 tu na anaota jua la saa sita mchana na hips zake ni kama alikalia hamira jua likiwa linawaka hivyo akaumka na kiuno ni kama yule mdudu mkali amaye sitaki kukumbuka alivyowahi nivimbisha uso anaitwa Nyingu.
Uso wake ni uso ambao kila dakika ukimwangalia unafikiri kuna kitu anataka kukuambia tena chenye kukupa furaha ya moyo na nyele zake hatumia hivi za naninihii yeye zake ni za kuzaliwa na ziliufunika vyema upande mmoja wa uso wake na kuniachia sehemu ya kuona jicho lake moja ambalo kun a kama mara tatu hivi nilidhani ananikonyeza lakini nikagundua hakuwa na lengo hilo ni papara zangu.
Nikawambia tu be honest sina haja ya tangazo na hapa nilitaka kuweka mtego wa kukubana. akanyayua kidole chake na kunibala midomo yangu na kuniambia mimi sio mtoto na wale sio mgeni wa mapenzi.
Nimekusikia muda mrefu na kuna siku uliwahi ongea na mdogo wangu mmoja akasema msalimie dada yule mdogo wangu ulikuwa ukimsaidia kazi fulani hivi kama unakumbuka..... wakati huo sikuwa na neno la kuongea na jasho jembamba naona linatirika kutoka sehemu mbalimbali za mwili wangu.
Akaunyanyua mkono wangu na kuanza kuukiss kwa mbembe za hapa na pale mie jasho likazidi kunitoka na nikashisi kama watu walikuwa wakiniona ninavyohangaika pale hotelin kwa mbalia akaniuma kidogo kwenye kidole kwa mshtuko nikapiga kelele stooooooooooooooooooooooooooooooooooooooop na kuruka kabla ya kugundua ilikuwa ni ndoto nililala hapa sebuleni na mkononi sikuwa nimenawa baada ya kula na huyu paka wetu alivyo fala alikuwa akiulamba mkono wangu.
Duuh ngoja niamke niende town kutafuta ndovu....... Nice weekend wazeee
Hizi ndoto bwana
Tangaza bure na blog hii, wasialiana whatsapp 0713317171
Soma kisa hiki facebook na maoni ya marafiki kwa kubofya HAPA
0 comments: