Soma jinsi sumuni inapobadilishwa kuwa mamilioni ya shillingi

22:41:00 Unknown 0 Comments

Dada mmoja alihitimu chuo na kutafuta kazi kwa muda mrefu sana kiasi cha kukaa mika 15 akiwa
hana kazi. Mbaya zaidi katika kipindi hicho alipata wakati mgumu namna ya kupata fedha za
kujikimu.


Siku moja akawa na elfu tano tu na akaingia katika hoteli moja ili aweze kupata chakula cha mchana, akaketi na kuagiza chakula chake.

Baada ya kuletewa akasali na kabla ya kula chakula wakaingia wazee watatu wakionekana wamechoka na wanajaa pia.Wakamwomba kile chakula nae akawapa kwa moyo mkunjufu.

Wakamwomba wamsalie naye kwa huruma akawajibu kuwa wao walihitaji kuombewa zaidi yake na akawa anajiandaa kuondoka, lakini kabla ya kunyanyuka wakampa hela ya koini ya zamani ambayo haina maana yoyote naye akaichukua na kuondoka zake.

Akaondoka zake na kwenda kwenye bustani moja pale mjini na kuamua kulala ili ajipumzishe
mchana ule huku njaa ikimuuma na uchovu wa kuzunguka akihangaika kupata kazi.


Akiwa kalala pale akaona kipande cha gazeti toleo la karibuni na kuona tangazo kuhusu hela ya koini
ya zamani iliyopotea katika jumba la kifalme mwaka 1992 na kama mtu angeiona hiyo hela angepokea zawadi ya shilingi million 100 za kitanzania.


Baada ya kuliona tangazo lile akaiangalia ile koini na kuona iko sawa sawa kama ya tangazo lile
kisha akakimbia mpaka sehemu alipoelekezwa na tangazo lile akapokea cheki yake ya shilingi
milioni mia moja na kurudi mbio mpaka ile hoteli ili awaone wale wazee watatu lakini wakawa
wameshaondoka.


Alipowauliza wale wahudumu wakampa barua aliyoachiwa na wazee wale na alipoifuingua ndani
iliandikwa:-


"mimi ni Mungu baba wa wenye matatizo, Mungu mwenye kujua matatizo ya kila kiumbe wake.
Hakuna mtu amtumainie bwana Mungu ataachwa ateseke katika maisha yake.

Mtu aishie kwa kumnyenyekea Mungu ataishi katika kivuli cha Baraka, mafanikio, ushindi, afya
njema, furaha na amani tele”


Baada ya kuisoma barua dada yule alijawa na furaha na kuondoka kurudi kwake akiwa na fedha
baada ya kukaa zaidi ya miaka 15 akiwa anasaka kazi na fedha bila mafanikio huku akizidi kumshukuru MUNGU wake


Funzo:

Umebarikiwa ule mkono unatoa zaidi kuliko ule unasopokea...


Mtumainie Mungu na maisha yako yatabadilika kuanzia darasani, kazini, nyumbani, mtaani na kila sehemu...
Sala kwa ajili yako:

Mungu atakufanyia miujiza ya Baraka katika maisha yako ndani ya mwaka huu, miujiza mikubwa na yenye furaha kuliko unavyotegemea na utafurahia maisha yako........ Amen

You Might Also Like

0 comments: