TAFADHALI SOMA INAKUHUSU NA ITAKUEPUSHA NA KIFO CHA FEDHEA

10:01:00 Unknown 0 Comments



Miezi sita baada ya kuhitimu masomo nilikutana na kaka mmoja ambaye tulishawahi kusoma nae shule moja miaka kadhaa iliyopita, na kwa wakati huo  alikuwa mfanyakazi wa taasisi fulani kiserikalini.

Taratibu tukajikuta tukianza kuwa marafiki ambao punde tena kwa kasi ya ajabu tukiwa wapenzi wenye hisia kali na msimamo wa kimapenzi baada ya mwaka mmoja.

Hali yake kimaisha hakiuwa safi sana yaani sio mtu wa kuweza kuwa na mipango mikubwa japo aliyamudu mahitaji ya muhimu kwake na tukaanza kufikiria kuja kuwa pamoja ila nikahisi itakuwa mzigo nikamwomba tujipange kwanza.

kipindi hicho rafiki zangu wawili walikuwa tayari wakiwa na biashara zao na wakiendesha magari mazuri sana. Wakati huo mimi ni mfanyakazi wa kujitolea katika shirika fulani la kijamii nikiangalia kama nitapata uwezekano wa kupata kazi.

shauku na hamu ya kuwa na maisha mazuri kama rafiki zangu ikaanza kuninyemelea na hatimaye kuwa moja ya ajenda muhimu katika fikra zangu kila siku. Msukumo huo ukanifanya nimfuate rafiki yangu ambaye akaniambia kuwa mie tatizo langu ni mshamba na muoga ndio maana sipati bahati.

Baaada ya kuidadisi bahati hiyo hatimaye akaniunganisha na mzee mmoja ambaye akaniahidi kama ningelala nae na kuamua anilingilie kinyume na maumbile basi angenipa fedha na gari na pia angenisaidia kupata kazi nzuri au hata kuwa na biashara nzuri.

Nikamfuata rafiki yangu na kumwomba ushauri akaniambia kuwa ni mchezo mzuri na wala sitakiwi kuogopa na kuwa hata yeye ndio siri ya utajiri wake na wala nisiwe na wasi wasi kabisa. Nikamfuta yule mzee na kumweleza kuwa kuwa ni kweli nimekubaliana nae na pia ndoto yangu ni utajiri na kuwa na maisha mazuri.

Nikaanza kujifunza ile tabia mbaya japo kuwa siwezi kuelezea kwani sipendi kukumbuka kabisa kisa  hiki Fuledi lakini nitajitahidi kuelezea japo sio kwa undani wake.

Kitendo kile  ilikuwa ni kama unyama usio na kifani na namwomba Mungu anisamehe sana kwani niligeuka na kuwa shetani. Baada ya uzoefu ule sasa nikawa sitamani aina yoyote ya mapenzi zaidi ya mchezo huo jambo lililonifanya niingie gharama kubwa ya kwenda mahospitali mbalimbali kila mwezi kusafishwa sehemu yangu ya haja kubwa.

Fedha zikazidi kuwa nyingi kwani sasa nikajigeuza na kuwa mfanyabiashara wa bidhaa hiyo na nikawa mtu wa matanuzi na sikuwa tena na wazo na yule mpenzi wangu aliyekuwa akifanyia serikalini.

Mwaka mmoja baadae nikaanza kuona dalili za ajabu kila nikikaa sehemu mara nione maji yamejaa, nguo nabadili zaidi ya mara nne kwa siku, sipandi daladala wala kwenda sokoni nikihofia kuchekwa watu wakiona maji na nikaanza kukosa raha kwani hata mtu nikimpa lifti kwenye gari langu pia naanza kuhofia maana nilianza kutoa harufu mbaya.

Kila hospitali niliyoenda mambo yakwa magumu na hali ya kunuka ikazidi na baadhi ya marafiki wakinikimbia na gharama za hospitali zikaanza kuwa kubwa. Nikaanza kuuza magari yangu na baadhi ya vitu ili nipate tiba na nikiwa na hamu ya kuwa kama binti yule wa zamani bila mafanikio ya kupona nikisafiri kwenda kenya, uganda na afrika ya kusini bila ahueni.

Mpaka ninavyoongea hapa ni mtu wa kusubiri kufa kwani nyama zimenitoka sehemu za nyuma na pia wanatoka wadudu wadogo wadogo wale kama funza huku nikinuka na uwezo umeniishia hata wa kuweza kulipia dawa nikiwa sina msaada na wale marafiki hawapo tena.

Wengi wetu sasa tumefikia kuona kama ni fashion na njia za kuwaridhisha wapenzi wetu na imefikia kudanganyana kuwa hips zinakuwa na unaonekana mjanja........ lakini amini msiamini niushamba.

Naomba Msamaha kwa MUNGU wangu kwani najua muda wowote nitakufa kwa maumivu haya na aibu niliyonayo sio kwangu tu hata kwa watu wanizungukao na Mungu wangu pia.

Naumia kwa kuwa hata nikifa sasa sijapata bahati ya kuwa dada mwema na naumia zaidi ndugu wanaoinizunguka na jamii nimewachafulia jina .... Nisameheni

Nawaomba dada zangu tuache tamaa na kamwe msije fikiri ni fashion au ujanja au ndio njia ya kuwafanya wapenzi wenu wawapende zaidi au kujipatia fedha bali ni ujinga na upuuzi wa kinyama wafanyao watu wasio na akili zao bali shetani akiwaongoza.

Jirekebisheni.

Naomba share ujumbe huu kumwokoa dada yako na janga hili.

You Might Also Like

0 comments: