"Uko wapi?"
Ujumbe wa JumapiliMungu anapokuuliza swali
Nimemwandikia ujumbe huu rafiki yangu sana ambaye anapita katika kipindi kigumu cha mpito ya masha yake. Nikaona ni bora nikupe nawe rafiki wa hapa upate kusoma na kuitumia fursa hii.
Tunavyosoma Biblia, Huwa napenda Mungu anavyouliza maswali. Hajiulizi yeye hapana ila yeye huwa na majibu ya maswali hayo. Bali hutuuliza sisi kwa kuwa hutaka sisi tupate uelewa wa maswali na majibu yake na kuyafanyia kazi.
Alimuuliza Adamu, "Uko wapi?" Kuna kipindi huwa hatujui tuko wapi katika Maisha yetu ya kawaida hivyo twaitaji sauti ya MUngu kutukumbusha wapi tulipo na kuweza kupata nguvu za kuishi vyema..
Alimuliza Musa, "Nini umekibeba mikononi mwako?" Mara nyingi kila tunachokihitaji na baraka nyingi tayari huwa mikononi mwetu lakini bado huwa ngumu kwa sisi kutambua hilo.
Alimuuliza Malaki, "Mtu anaweza mwibia Mungu wake?" katika Maisha ya sasa imekuwa rahisi sana kwa sisi kutumia muda wetu kwa kila jambo lakini tukamsahau Mungu.
Alimuuliza Ezekiel, "Mifupa hii inaweza ishi?" Kuna wakati unaweza pita katika nyakati mbaya nakujiona kama mfu lakini Mungu anakukumbusha kuwa bado uko salama na mambo bado mazuri kwako.
Alimuuliza mtu aliyepooza, " Unataka kupona??" Mungu tayari anajua unahitaji kupata ahueni ya Maisha yako ila anasubiri kwanza wewe ulione hilo na kulitamka kwa kunywa chako
Alimuuliza Abraham, "Kuna jambo lililo gumu kwa Mungu?"
Nafikiri unavyozidi kuendelea kuishi katika dunia hii. Hata kama mambo yakawa magumu au yakutisha kiasi gani, hakuna jambo linalomshinda Mungu.
Nakuombea wewe leo rafiki zako na ngudu zako
Jumalipi Njema
Tabasamu na Fuledi
whatspp 0713317171
0 comments: