HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 20

14:29:00 Unknown 0 Comments

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

Season 20

ILIPOISHIA JANA

Tulikaa kwa dakika kadhaa kukijadili na kutathmini juu ya azimio hili la kwanza unywaji wa pombe kupita kiasi na kisha tukagundua kuwa ulevi ni noma na kukubaliana kuachana na azimio hilo la kwanza kwani pombe zingetuua na sio azimio la kulichekea kabisa..
Tukiwa tunafikiria azimio la pili mara simu zetu zote ziliita kwa pamoja tena namba ngeni hivyo tukawa tukizitazama tu na ghafla mlango ukagongwa kwa fujo. kwa kuwa mwakibubu alikuwa hayuko poa nikasimama na kwenda mlangoni.
Ile naufungua ule mlango nilichokutana nacho..................................................


ENDELEA

Ile naufungua ule mlango nilichokutana nacho kilinifanya niduae kwa sekunde kadhaa na kisha nikamgeukia mwakibubu kama nilitaka kumkonyeza kitu lakini nikanshindwa baada ya polisi kuniuliza,
 " wewe ndio Mr Mwakibubu?" Na hata kabla sijawajibu binti mmoja mwenye mvuto wa kipekee alipokea kwa kusema ..... " Afande sio huyu amwite rafiki yake"
"Unajichelewesha nini hebu mwite mdwanzi mwenzako, yaani mnafanya matukio na mnafikiri hapa ndio mmejificha? Muulizieni Osama pamoja na kujificha lakini alidakwa sembuse nyie vijiarifu???
Nilishaanza kutetemeka na wakati nageuka bwana mwakibubu hakuwepo pale ikanibidi niende mpaka karibu na mlango wa chumba chake na kumwita akaniambia kuwa anakuja ngoja avae kwani muda huo alikuwa na pajama.
Dakika moja baadae alitoka na hakuruhusiwa kuongea chochote akapandishwa kwenye gari lillokuwa na polisi wanne ndani yakena kuanza safari ya kupelekwa kituo cha polisi kati kwa mahojiano zaidi. Nilifunga milango na kuwasha gari kuanza kuwafuata taratibu mpaka nilipofika pale kituoni  na kukuona alishahojiwa  na kuandika maelezo.
Kesi iliyokuwa ikimkabili bwana mwakibubu  ni ya kumtukana na kumdhalilisha yule dada na kumtishia kumpiga pia ilidaiwa kuwa alimwibia simu yenye thamani ya shilingi milioni moja na tisini elfu na kusababisha uharibifu wa mali nyingine kama vile ipad, laptop pamoja na kuukata kumkufu wake wa dhahabu.
Jambo la ajabu ni kwamba mwakibuubu alikuwa haelewi lolote na hata alipohojiwa juu ya namba iliyompigia hakuweza kuionesha kwa kuwa haikuonekana jambo ambalo lilizidi kumweka bwana mwakibubu hatiani.
Jumla bwana mwakibubu alitakiwa alipe shilingi milioni mbili na nusu kama fidia kwa yule dada ili yaishe pale. Ilimbidi akae pale lupango kwa zaidi ya masaa matatu wakati mimi nahangaikia suala la dhamana ili atoke na tujadili nini kifanyike maana fedha hizo zilikuwa ni nyngi mmno za kukufanya mtu umiliki hata kabajaji kadogo.
Nilifanikiwa kumchukulia dhamana na tukaanza safasi ya kurudi nyumbani huku bwana mwakibubu akiendesha gari kwani muda huo mmi nilijisiia uchovu. Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza toka tufahamiane na mwakibubu kumwona akimwaga chozi kama mtoto mdogo akilalamika juu ya lupango kuwa sio sehemu salama na akimlaumu yule dada kwa kumtengenezea kesi.
Kwa upande wangu nilihisi kuwa alikuwa akinificha kitu kwani haiwezekani apigiwe simu na chamdoli halafu aende kwa yule dada na ghafla ibadilike kuwa sinema ya ngumi.... Haikuniingia akilini.Sawa matatizo tunayo na tunatakiwa kukabiliana nayo ila  nikaanza kumwona bwana  mwakibubu  kama vile anaanza kupanic.
Yakazuka mabishano makali baina ya mimi na mwakibubu kwani mwakibubu akaona kuwa mimi simwamini na kwa upande wangu   nikawa mkali kwani nilishaanza kuchoka na drama zetu ambazo sasa kila kukicha zinatuletea aibu au matumizi makubwa ya fedha.
 Tukiwa katikati ya mabishano hayo ghafla nilishtushwa na mshindo mkuu ambao hata kabla sijananyua mdomo nilipoteza fahamu.
Saa moja baadae nilishtuka nikiwa hospitali na tukiwa tumezungukwa na watu ambao kwamwe sikuweza kuwatambua na nakumbuka maneno ya kwanza kuyasikia kutoka kwa watu wale  ilikuwa ni kutoka kwa dada mmoja aliyesema, " Jamani huyu si baba pachu na yule ni rafiki yake mwakibubu?"
Nilishangazwa sana na nilipojaribu kujitazama tulikuwa tumechafuka vumbi kama vinyago na huku tukitokwa na damu baadhi ya maeneo. Mwakibubu alikuwa wa kwanza kusema, " Duh kaka namshukuru Mungu umeamka maana nilihisi ushatutoka kaka..."
Nikaanza kumhoji nini kilitokea?
" Kaka pale wakati tunabishana ghafla kuna gari dogo lililotea mbele yetu nami katika jitihada za kujiokoa nikajikuta nimeingia kwenye korongo..... Pole sana rafiki yangu ila namshukuru Mungu tulifunga mikanda maana bila hivyo sijui leo tungekuwa mtaa gani huko ahera..." alimaliza kuongea na kuanza kulia
Nikatazama upande wa pli na kutazamana na yule dada aliyesema ananifahamu nikamuuliza ananifahamu vipi? maana pale nilikuwa sina simu na nilihitaji nitoe taarifa kwa mke wangu.Dada akanijibu kuwa ni rafiki na mama pachu na kuwa yatari ameshawasiliana na mama pachu na yuko njiani anakuja kwa hiyo tupumzike..
*********************************************************************************************
Mama pachu baada ya kupigiwa simu na shoga yake alikurupuka na kwenda kituo cha daladala, akiwa ndani ya gari kuelekea hospitali huku akiwa na mawazo mengi na akijiongelesha kuhusu hali ya mimi na rafiki yangu mwakibubu  pembeni yake alikaa bibi mmoja ambaye alionekana  hajui wapi analekea.
Bibi yule alianza kumhoji mama pachu, " Vipi mjukuu wangu mbona unajisemesha mwenyewe haya niambie yapi yamekusibu jioni hii?"
" Acha tu mama yangu, nimepigiwa simu kuwa  mme wangu na rafiki yake  mwakibubu wamepatwa na ajali mbaya na muda huu wako hospitali yaani nimechanganyikiwa sana mama yangu" aliongea mama pachu

Lile jina mwakibubu lilimshtua sana yule bibi na kwa uhakika zaidi yule bibi akamuuliza tena mama pachu, " Niambie umesema rafiki wa mme wako anaitwa nani?"
"Mwakibubu"  mama pachu alisisitiza
"Kweli duniani kuna mambo huyu mtu nilikuwa namtafuta tangu jana maana nina maagizo yake." aliongeza bibi
"Maagizo gani hayo basi twende wote hospitali ukaonane nae" aliongeza mama pachu na kimya kikawatawala kwa dakika kadha mpaka walipoingia wodini.
Walipofungua tu ule malngo mwakibubu aliruka toka kitandani nakufanya wodi nzima ibaki katika taharuki kwani sura aliyoiona ilkuwa ni ya bibi GUSA UNATE jambo lililonishangaza sana mimi kwani nilizisikia hadithi zake ila sikuwahi kuonana nae.
Mwakibubu akaanza kumfokea yule bibi na kumwambia, " Yaani wewe bibi haijatosha tuu, Umenilaghai na kutaka kuniibia,  umeenda ofisini umeniharibia kazi na sasa unanifuata huku? Nashukuru umenirahisishia kazi ya kukutafuta kwani leo nakuua hapahapa na mochuari iko karibu hivyo hawatapata taabu ya kukupeleka"
Bibi huyu alionekana kwa mpole kuliko nilivyohadithiwa na aliongea maneno machache tuu yenye hofu ndani yake, " Mjukuu wangu hata mimi nilikuwa ninakutafuta....."  hata kabla hajamaliza mwakibubu alimzima kauli kwa kumwambia, " aaah sasa kumbe bado unanitafuta hivyo tunatafuana?? Ok  sasa subiri"
Alinyanyua mkono ili ampige lakini aliishia kutoa kelele za uchungu kwani mkono ulikuwa umevimba sana na una maumivu makali kwa ndani. Bibi gusa unate alisisitiza kuwa awe mpole na amsikilize kwa makini kwani ana ujumbe wa wake na wa mimi baba pachu.
Kipindi hicho mama pachu alikuwa katoka kwenda kufuatilia dawa ambazo tuliandikiwa hivyo bibi gusa unate alipata wasaa mzuri wa kutueleza nini kilichomleta pale.
" Wajukuu juzi usiku nilipigiwa simu na namba ambayo sikuitambua na ilinipa maagizo ya kuwa nikutafute wewe mwakibubu na kukutahadharisha kutotumia usafiri wa aina yoyote na kutulia nyumbani bila kutumia kilevi cha aina yoyote ile.....
 Akaendelea kusema, na pia namba hiyohiyo ilinisisitiza kwa meseji kuwa nikichelewa mkapata tatizo nitakuwa matatani, nimezunguka hapa mjini namba yangu ukawa huipokei na pia ofisini kwako wakakataa kunionesha unakoishi hivyo kwa bahati nzuri tu nikiwa ndani ya gari ndio nikakutana na mke wa huyu rafiki yako"
"Jamani hi namba inanitakia nini mimi bibi wa watu ambaye nimejiishia tuu nakula pesheni yangu taratibu?" alihoji bibi gusa unate.
Ni wakati huu ambapo bwana mwakibubu alicheka bila nukta wala koma huku akimwambia bibi wewe si mganga wa afrika mashariki na kati?
Yanakusibu yapi mpaka umwogope huyo kwangua vocha? Si umpe ule moshi wa pilipili? Na simu yako ungeidumbukiza kwenye kile chungu chako?
Bibi alionesha hali ya kuzidi kuchanganykiwa na kusema, "Mwanangu usicheke mbele ya kifo, mimi nipo mashakani hapa na siwaachi kwani huyu mtu anaonekana ananifahamu na ana roho mbaya sana, hebu fikiri kila nyendo zangu anazijua... hebu kwanza nishikie hii simu yangu.
Wakati akaiwa anaunyoosha mkono ili kumpa simu bwana mwakibubu ghafla simu ilianza kuita  ...........................

Je simu hiyo ilipigwa na nani na ilimtaka nini bibi gusa unate?

Usikose kisa hiki jumatatu jioni


Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu kwa udhamini wa Gracious HOUSE of CAKES watengenezaji maarufu na waliobobea wa keki za aina mbalimbali kwa hafla mbalimbali waliopo jijini Mbeya na wanapatikana kwa namba 0767218014

Nawe waweza kuwa mdhamini wa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

share, like na comment

You Might Also Like

0 comments: