Hebu fikiria kuanzia jumatatu wewe unahangaika na kazi ukijaribu kujituma ili uongeze ufanisi pamoja na kuonesha mfano mzuri kwa wenzako pale kazini.

11:43:00 Unknown 0 Comments

Kuna mambo ni ya msingi sana kuyafikiri kipindi uko nyumbani kwa mapumziko ya mwishoni mwa juma.

Hebu fikiria kuanzia jumatatu wewe unahangaika na kazi ukijaribu kujituma ili uongeze ufanisi pamoja na kuonesha mfano mzuri kwa wenzako pale kazini.

Na kama haitoshi unajituma sana kufanya saving ya kutosha ili angalau uje kufanikiwa kumiliki kagari kako, biashara yako au hata kajumba kako.

Na kumbuka juhudi hizi unaanza nazo mwanzo wa mwaka mpaka sasa kwa moto huo huo ukiwa na imani ya kuja kuwa na familia yenye mafanikio na maisha mazuri.. wewe si ndio utakuja kuwa kichwa cha familia bwana? hivyo lazima ujitume..

Na pia una kabinti kako nako kako moto sana ili ukamtambulishe kwenu na muweze kuanza maisha yenu ya kuwa pamoja kwani anaona kama mnachelewa na muda unazidi kwenda kuanza kuijenga familia.

Kule kijijini umemwacha baba na mama wakihangaika na kilimo na bado wanamatuaini makubwa ya kuwa siku moja utawaokoa angalu nao wafurahie maisha mazuri kutoka kwa mwanao.

Wakati huo huo upo busy sana sana kunyemelea videmu vya hapa mtandaoni ili angalau uweze kuosha nyota yako na kuruka navyo kwani picha zao zinakupa wehu.

Sasa basi baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu bila mapumziko unaamua weekend moja kwenda kupumzika ukiwa na huyo binti wako sehemu moja muhimu sana kwenu i mean hoteli moja nje ya mji.

Mkiwa huko anaanza kukupa mawazo yake na mipango mingi sana ya jinsi mtakavyoishi kwa kuraha mkiwa na familia yenu wawili na mafanikio mengine ya kifamilia.'

Unafurahi sana sana na ukaona kuwa hukukosea kuwa na binti huyu na unalishukuru hilo sana. Basi kwa kuwa muda huo mlikuwa chumbani unaamua kutoka zako na mpenzi wako na kwenda matembezi kuangalia mandhari ya ile sehemu mliyofikia.

Haujaanza hata kuzitazama zile bustani za hotel hiyo mpenzi wako anaanza kulalamika ya kuwa tumbo limembana na anahitaji kurudi haraka kulala ili apumzike na kwa mbaali kuna jamaa anakuja upande wenu.

Wewe haujali sana unamsaidia kumpeleka ndani ila yeye anaonesha naweza kwenda peke yake. Sasa ukiwa pale jamaa anakukaribia na kuanza kukupa vibao vya uso, mateke ngumi na wewe unajaribu kujinasua na yeye anazidi kukupa kelebu za haja.'

Baada ya wewe kujiokoa na wasamaria wema kuja yule jamaa anaanza kukulalamikia kwa kutembea na mke wake wa ndoa mabaye ana watoto wawili na jamaa na kuwa jamaa yeye huwa anasafiri sana mikoani na kumwacha mkewe mjini.

Kwa hasira unakimbia mpaka chumbani na kuona binti kashasepa na dakika chache baadae unapokea ujumbe wa sms kuwa "Samahani baby kwa kila kitu"

Sasa katika hili wewe utachukua maamuzi gani?

Je ndio utakuwa mwanzo wa stress na kuanza kuharibu hata zile saving zako?
Utaanza kuwachukia mabinti kutokana na hili?

Utajilaumu kwa kwa kuwa na mahusiano na mtu usiye na historia naye vya kutosha?
Au utabadilisha style yako ya maisha maana pia waonekana ni mtu wa kuwanyemelea watoto wa facebook ambao pia huna uelewa nao vya kutosha na ambao pia wanaweza
 kukuletea janga kama hili lililokukuta?

You Might Also Like

0 comments: