Bibi Gusa unate alicheka zadi na kusema ama hakika mjini shule kwanini nakuwa mzee ningeanza kampeni hii miaka ya nyuma hivi sasa ningekuwa namiliki mjengo wangu wa ukweli hapa mjini kisha akaanza kujongea kwenye kibanda cha kutolea fedha.

15:59:00 Unknown 0 Comments

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

Season 28

ILIPOISHIA JANA


Bibi Gusa unate alicheka zadi na kusema ama hakika mjini shule kwanini nakuwa mzee ningeanza kampeni hii miaka ya nyuma hivi sasa ningekuwa namiliki mjengo wangu wa ukweli hapa mjini kisha akaanza kujongea kwenye kibanda cha kutolea fedha.

Akiwa kasimama anasubiri kupokea hela yake kutoka kwa muhudumu wa kibanda kile mara simu yake iliita...........

ENDELEA

Akiwa kasimama anasubiri kupokea hela yake kutoka kwa muhudumu wa kibanda kile mara simu yake iliita,  bibi nalipoiangalia na kugundua ni simu ya chamdoli na kuwa wakati huo alikuwa amekiuka maagazio yake aliyopewa na chamdoli basi aliizima simu ile haraka na kuchukua hela kisha akatimka.

Akiwa njiani aliendelea kuumiza kichwa kwa mawazo juu ya hatma yake na huyo chamdoli na kuwa ni mtu au pepo wa aina gani asiyekuwa na simile zaidi ya kuharibu mikakati ya watu.
Na pia aliwaza kuwa hivi sasa kampotezea kabisa bibi ule utaratibu wake wa kujipatia fedha kama hapo awali na kuwa sasa hivi bibi amekuwa kama mtumwa wa mtu asiyefahamaiana naye wala kumwona.

Bibi alikumbuka jinsi alivyopewa adhabu ya kudeki bwalo baada ya kukutwa akikojoa eneo la jeshi, akakumbuka jinsi alivyotaka kupelekwa polisi baada ya kukimbiwa na mwakibubu pale hotelini na kutakiwa kulipia chakula na vinywaji ambavyo vyote alikuja kulipiwa na namba hiyo ngeni jambo lililomfanya aingie katika njia ya mahangaiko..

Akafikiri jinsi alivyoanza tabia ya kunywa pombe kwa hofu na hata kutokuwa na uhuru na simu yake akihofia kupigiwa na chamdoli na hata alivyopoteza wateja wapya kwa kuhofia kila namba ngeni na zaidi ni hili la kurudisha fedha zote alizowahi kuzidhulumu, kisha akajisemea moyoni, " Hapa ni kugangamala tu... mjini mipango"

Alipomaliza kufikiri hayo alikuwa tayari kafika nje ya hoteli moja kubwa na ya kisasa hapa jijini mbeya na kwa kawaida ni sehemu yenye kutembelewa na watu wenye fedha zao wakija kwa ajili ya vikao vya kibiashara au kupumzika baada ya kazi.

Bibi gusa unate akachagua meza moja tulivu na kuagiza kinywaji kimoja kikali sana na barafu zake na kisha akawa anasoma jarida moja lililokuwa mezani. Bibi alionekana kupendeza sana kwa mavazi aliyovalia kwani yalimfanya anonekana ni bibi mmoja mwenye fedha zake na amekuja kupumzika pale baada ya kazi nzito za siku.

Kijana mmoja aliyekuwa amekaa meza ya jirani baada ya kuvutiwa na manukato ya bibi huyo pamoja na mpangilio mzuri wa mavazi na kwa jinsi bibi alivyo, kijana akaona isiwe taabu aombe kukaa pale kwani hata kama ungefanikiwa kumwona bibi pamoja na uzee wake ule, lakini ungekubali kuwa umbo lake lilimfanya aonekane ni mama wa makamo.

Kijana huyo baada ya kuomba na kukubaliwa na bibi kukaa pale, alianza kwa  kujitambulisha jina lake kuwa anaitwa shukurubu na ni kijana aliyejiwekeza katika biashara ya mitindo na mavazi na kuwa ana maduka mengi sana ya nguo ndani na nje ya jiji la Mbeya.

Wakati huu bibi gusa unate alijifanya kutulia sana na kumsikiliza kijana huyo ambaye alishamwagizia bibi kinywaji kingine na bibi akawa kavutiwa na style ya shukurubu. " Asante sana kijana, mimi naitwa Grandma G kama wengi waniitavyo na hapa Mbeya nimekuja kutafuta fursa mpya za uwekezaji nikitokea nchi jirani ya zambia but here is my origin namaanisha Tanzania " Aliongea bibi kwa kiswahili cha shida 

"Ok karibu sana basi nitapenda kuwa mwenyeji wako kwa siku zote utakazokuwa hapa Mbeya kama hutojali" aliongea shukurubu huku akijiweka sawa kwa kujidai 
" oooh Asante,I wish iwe hivyo ila hapa nimestaki kwa muda kwani ninatatizo na kadi yangu ya benki (masta kadi) kwa ajili ya malipo, hivyo nitatakiwa kukaa hapa mpaka  nipate fedha za kwenda dar mara moja then nitarudi hapa nikiwa na muda mrefu zaidi wa kuongea na baadhi ya watu ambao tayari nimeshawaweka katika mpango kazi wangu" aliongea bibi huku akiinyanyua glass yake kuipeleka kinywani

"Nafikiri isiwe taabu kwani ni kiasi gani unafikiri kingeweza kukusaidi mpaka kufika dar na kufanya kazi zako pengine naweza kukupa na ukirudi utanirudishia si wajua sehemu kama hizi twakutana na marafiki wengi ambao hugeuka na kuwa zaidi ya ndugu? " aliongeza shukurubu
" Wow!!  thanks that's  so nice of you, hivi ni vijana wote wa hapa mbeya wako kama wewe? Utafanikiwa sana kwa wema huu na nikirudi nitakutafuta tukae vizuri na kujadili waweza simamia miradi yangu nitakayoianzisha hapa mbeya,Nafikiri milioni moja inaweza kunisaidia kwa siku hizo mbili nikiwa dar" alimaliza bibi

Shukurubu alimalizia funda la mwisho na kumuaga bibi kuwa anaenda ATM mara moja kisha atarudi punde.

 Akiwa njiani shukurubu alifurahi sana  na kuona sasa katika mitego yake yote ya kunasa wake za watu na kumweka mjini huu ulikuwa ni babu kubwa kwani sasa atamweka mkononi bibi mwenye hela za kutosha na ambaye ni mwekezaji kutoka zambia.

Nusu saa baadae shukurubu alirudi   na kumkabidhi bibi fedha taslimi shilingi milioni moja na baada ya maongezi kidogo na kubadilishana mawasiliano bibi alimwomba bwana shukurubu aende akapumzike na kumwacha shukurubu akiendelea kunywa kwa furaha ya kukutana na mwekezaji.

Bibi alizunguka upenuni mwa eneo hilo na kupanda bodaboda mpaka Tandika tulale Guest House na kuanza kupata vyombo huku akimpa ofa kila mhudumu pale na wote walifurahi kwani ilikuwa ni muda tangu bibi aonekane eneo hilo.

*********************************************************************************

Siku ya pili asubuhi baba pachu aliamka na baada ya kazi za hapa na pale akisaidiana na mkewe na ukizingatia siku hiyo ilikuwa ni jumamosi na kila mtu yupo nyumbani basi akamuaga mkewe kuwa anenda kumsalimia bwana mwakibubu kwani siku kadhaa hawajakutana.

Alifika kwa mwakibubu na kwabahati mbaya hakuwepo nyumbani na baada ya kuwasiliana naye akaamua aende kumfuta mwakibubu ambaye alikuwa yuko kuogelea katika hoteli moja yenye bwawa la kuogelea nje ya mji. Muda mfupi baadae walikutana  na kuanza mazungumzo yao ya kawaida.

Lakini mwakibubu alihoji zaidi juu ya simu aliyopigiwa na mkewe jana yake usiku kuwa aliota ndoto mbaya ingawa baba pachu alisisitiza kuwa ni ndoto tu na pengine mama amigo alitaka kumtahadharisha mwakibubu asije kuwa na mchepuko wakati yeye yuko kijijini.

" baba pachu unajua mimi namshukuru Mungu sana kwani nina zaidi ya siku kadhaa nikiwa nimepumzika bila ya chamdoli wala nini na ninalala kwa raha wala sinywi tena ile mipobe umiza kichwa na huwezi amini najiona  kama nina nenepa kwani sina cha kuniogopesha tena" aliongea mwakibubu

" kaka yaani mimi nafuraha zaidi kwani hata ile furaha ndani ya nyumba imerudi baada ya kupotea kwa muda na hapa kati nilianza patwa na hofu maana mama pachu naye alikuwa na hofu sana nikajua amehisi kitu kwangu na ananifuatilia lakini naye katulia sasa hivyo mambo mazuri sana" aliongeza baba pachu.

Walikaa pale na kuagiza chakula cha mchana na kuendelea na mazungumzo huku kila mmoja akiwa na furaha. Kwa kuwaangalia siku ya leo mwakibubu na baba pachu kwa mara ya kwanza walionekana kuwa na furaha tofauti na hapo awali.

Wakiwa wamekaa pale kuna meseji iliingia kwa baba pachu na alipoichukua na kuisoma ghafla aliruka na kuitupa simu chini huku akipiga kelele,  Kakaaaaa!!!! kakaa!!! duuuuh!!!! kaka!! kaa!!! na kisha  akaanza kukimbia kuelekea kwenye gari na kuisahau ile simu.

Mwakibubu aliichukua ile simu na kuiona ile meseji kutoka kwenye namba ya chamdoli ikiwa imeandikwa, " Mambo mpenzi, yaani toka mara yetu ya kwanza kuongea kule iwindi leo nimeshuhudia unafuraha tena, nitakupigia usiku usizime simu... kuna kitu cha muhimu nataka kukuambia mida ile ile kama ukiwa kule   iwindi"

Mwakibubu alinyanyuka na kuanza kukimbia akimfuata baba pachu ambaye alikuwa kaishiwa nguvu na pozi wakati mwakibubu akiwa anampa simu mara nae simu yake ikaanza kuita.

Ile anaipokea tu ile simu .................................................

Usikose mwendelezo kisa hiki kesho jioni

MUHIMU

Neno kutoka kwa mdhamini

Gracious HOUSE of CAKES tunakukaribisha Forest ya zamani.. nyuma ya Green lounge pembeni ya Penge kwenye duka letu. utajipatia Cakes za kila aina. Magic popcorns na suprises cup cakes. tunapokea oda hata za mwakani sababu tanapenda kufurahi na wewe. tunaanda bday party kwajili ya watoto na hata watu wazima kwa bei nzuri tuu.. kaa hunanafasi yakuja pia usipate mawazo sababu tunakuletea utakacho mpaka ulipoo. KARIBUNII SAANAA.

KUMBUKA

Kama unataka kusoma visa vya mwanzo tafadhali tuma Simu ya Ajabukwenda whatsapp namba 0713317171

Share, like Simu ya Ajabu na comment ili kisa kingine kiwahi kuletwa

OMBI

Unaweza kuwa nawe mdhamini wa simulizi hii tamu kwa kuwasiliana nasi kwa kuandika neno UDHAMINI kwenda whatsapp namba 0713317171

You Might Also Like

0 comments: