Ila kuna mambo mengine yanaboa sana hapa mtandaoni

11:48:00 Unknown 0 Comments


Hebu fikiria unaamka asubuhi na kukutana na meseji kutoka kwa kabinti ambako umekuwa unakanyemelea kwa muda mrefu na hujawahi hata kukaambia kuwa unakataka.
Kanakutumia meseji " Fuledi mambo vipi wangu, nimekuja mbeya plz naomba fanya juu tuonane mimi nimefikia hotel x na mida ya usiku nitakuwa free i want to see you nina zawadi yako"
Mzee najifanya kuwa busy kisha namwambia ok nitacheki kama kuna uwezekano wa muda kisha nitakuambia usijali.
Hii yote inakuwa kumwonesha kuwa nami niko tight sana kumbe hata angesema niende muda huo ningeenda.
Basi jioni nikamcheki akaniambia ndio anatoka field anangia hotelini hivyo baada ya dakika kama 45 niende atakuwa kajiandaa.
Kijana sio kujiandaa huko, kula mapafyumu kama kichaa nikapitia kwa jamaa yangu akaniazima kama 70 ili ninunue mafuta ya gari kama ya elfu 20 na kwa mbeya hapa ukiwa na 50 lazima usimamie show ajue kweli wewe mzee uko juu.
Nimefika pale akaomba tule wote dina, nikakubali na kumpeleka hoteli nyingine lakini muda wote huo mie najipanga najua toto limeingia line lenyewe .... kwa kifupi yuko kitonga yaani ni mteremko tuu.
Tumekula tumezungukan bar mbili tatu akaomba turudi hotelini kwake ili anipe zawadii.
ndugu msomaji usinionee gere
Ebwana nafika hotelini ananipeleka mpaka chumbani kwake ananiweka kitandani na ananambia nifumbe macho kisha anasema sapraaaaaaiz!!!!!!!!
Ile nafumbua macho ananipa zawadi ya soksi pea mbili eti hizi nimekununulia nilviyoenda dubai yaani nikaona zitakufaa sana plz take it nenda home and see you kesho maana boyfriend wangu kanipigia simu yuko njiani anakuja
Soksi my fooot nimezitupilia huko hapa nawaza jinsi ya kulipa 70 ya watu...
Madem wengine wadhalilishaji hapa mjini

You Might Also Like

0 comments: