" Mjukuu wangu chamdoli kwa hili nisamehe tu, Give me only this one last chance nitengeneze hela ya mwisho" kisha akazima simu na kurudi huku akiwa kaokota jiwe moja laini sana akilipekecha mkononi.

14:58:00 Unknown 0 Comments

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

Season 27

ILIPOISHIA JANA

Baada ya akili kutulia segito au kama alivyozoeleka kwa jina la mama kiduku alisimama na wakampigia huyo mama ambaye alikuwa akiishi nje kidogo ya jiji la mbeya na kukubaliana kuwa siku ya pilia wakutane mahala fulani bila kumwambia nini walikitaka.

Nesi mwalikumba liachana na yule mama kiduku na kurejea nyumbani kwake ambako alimkuta bibi keshazinduka kutoka kwenye usingizi uliosababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi.

Kabla ya kuufungua mlango Nesi mwalikumba alipokea ujumbe uliomtaka...........
ENDELEA

Kabla ya kuufungua mlango Nesi mwalikumba alipokea ujumbe uliomtaka kupumzika na kumpatia bibi simu kwani alikuwa kafanya kitendo cha kishujaa ingawa alitakiwa afanye hata kabla ya kupigiwa simu na ukamkumbusha kuwa ni wajibu wake kama nesi kuwa na maadili mema katika kazi yake na kurejesha furaha za watu kuliko kuwaumiza.

Alipofungua mlango alishangaa kumkuta bibi akiwa jikoni yaani tayari alishachukua kuku nusu aliyekuwa kabaki akisubiri kupikwa weekend wakati nesi akiwa mapumziko na muda huu bibi alimchemsha kuku huyo na kujipendelea supu moja matata sana.

" Mjukuu yaani wewe unaishi kama kipindi mimi niko huko Uruguay nasomea Swimming yaani nilikuwa nakula vitu kama hivi baada ya kupiga vyombo vya kutosha jana yake...

Vipi mbona ulinifungia? Halafu nimefikaje hapa? maana mara ya mwisho nakumbuka nilikuwa nakula vyombo vyangu sehemu nikiwa na watoto wa mjini.... eeeh haya nieleze umetoka wapi? aliongea bibi huku akinyanyua paja la kuku na kuliweka mdomoni.

Nesi mwalikumba alishangaa kwa muda na kisha akamuuliza,

" Hivi wewe ni bibi wa namna gani? kwanza umeniletea matatizo na pili umenifanyia mambo ambayo kamwe sitakuja kuyasahau na sijui yataishaje maana nimechangayikiwa.

Na kama haitoshi huyu aliyeniambia nikutafute ni nani? Tafadhali hebu nifungue maana hadi sasa sielewi na inaonesha ananifahamu vizuri na hiyo dawa uliyoniambia unaniletea iko wapi?" Alihoji nesi mwalikumba huku akionesha dalili za kuchoshwa na bibi gusa unate.

"Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha mjukuu wangu, hii ni dunia mi mwenye hapa nilipo ni most wanted yaani usinione niko hivi na muda wote niko vyombo nipo kwenye shuruba ndefu sana.

Unamfahamu vizuri chamdoli wewe? Unabahati sana maana muda huu wewe nyota yako ingekuwa ilishafifia" aliongea bibi huku akimalizia pegi ya mwisho ya supu yake kwenye sufuria.

Niambie maana simwelewi kabisa na sijui anataka nini katika maisha yangu yaani naomba Mungu mambo haya yasijekufika kazini mbona nitakufa? aliongea mwalikumba

"he he he he nicheke mie yaani wewe na unesi wako unatishika? tena nitakuajiri kwenye zahanati yangu ili ......." hata kabla bibi gusa unate hamaliza kuongea simu ilipigwa kwa nesi mwalikumba.

Nesi alipoiona namba ile kuwa ni ya chamdoli akasimama kwa haraka pale alikokuwa amekaa na kumpa bibi. Ni wakati huu sasa nesi mwalikumba alipogundua kuwa duniani hakuna mtu mwoga kama bibi gusa unate.

Kwani alipokea simu na kujfanya amezidiwa na tumbo na hawezi kuongea na kujilaza kwenye kochi, lakini mpigaji alisisitiza kuwa nilazima bibi apewe simu hivyo bibi akawa hana jinsi zaidi ya kuipokea hiyo simu.

" Safi safi safi sana, hivi wewe bibi unanitafutia nini? Na nilikuambia ufanye nini na wewe unafanya nini? Sasa ili kukuonesha kuwa mimi ni nani ondoka hapo ulipo bila kumwambia kitu huyo dada na kisha nenda mpaka nyuma ya nyumba hii nina maagizo yako muhimu ." alimaliza chamdoli huku akiwa bado hewani

Bibi aliondoka na kuufungua mlango huku akitoa ishara kwa Nesi kuwa amsubiri na kuzunguka nyuma ya nyumba ambako alimpiga mikwara mizito ikiwa ni pamoja na kurudisha fedha zote alizozichukua kwa yule dada wa tikisa mdodo ambaye yeye alikuwa akishika lile nyoya kila aendako na kusubiri miujiza bila ya kufanya kazi pamoja na wengine wote aliowahi kuwaibia kisanii na kisha chamdoli akakata simu.

Bibi alichanganyikiwa zaidi ya kawaida na kurudi ndani ambako alimwachia simu yule nesi na kusema atarudi na kisha akatoka kwa mbio zilizomwacha nesi akiwa na maswali yasikyokuwa na majibu na kuamua kuufunga mlango wake na kupumzika.

******************************************************************************************

Bwana mwakibubu alikuwa kanogewa na filamu moja nzuri na wakati huo kashaanza kusinzia akiwa sebuleni kabla ya kushtushwa na simu iliyotoka kwa mke wake mama amigo aliyeko kijijini kuwa alioteshwa ndoto mbaya sana juu ya mme wake usiku uliopita.

"mme wangu uko salama lakini? kwa upande wangu sio safi kabisa, maana nimeoteshwa ndoto kuwa wewe na rafiki yako baba pachu mlikuwa kwenye shimo moja refu mkiwa mnaomba msaada lakini kila nilipojaribu kuwasaidia kuna mtu nisiyemuona alinishika na kunizuia kuwarushia kamba.

Kama kama haitoshi nilishangaa kumwona mama pachu akiwa na dada mmoja ambaye simfahamu na bibi mmoja wakicheka sana tena kwa dharau kuna nini kinaendelea mme wangu? maana hii ndoto inahisia na inanitisha sana " alimaliza mama amigo

" ha ha ha mama amigo nawe hujaacha vituko vyako? hiyo ndoto tuu na utakuwa umenimis hebu niambie kwanza unarudi lini maana nyumba sasa hivi ina vumbi zaidi ya makumbusho, nimezirudia nguo zote na sasa nimebakia na kanzu tuu hapa, utarudi lini au nije kukusalimia?" alihoji mwakibubu

" Hapana ila mimi bado nina hisia na hicho kitu nilichoota na naomba kuwa makini sana huko mjini baba amigo, na kuhusu huku bado kidogo kwani lile shamba kubwa hatujalianza kwani tulisimama siku mbili si wajua mkwe wako anaumwa?" Aliongea mama amigo

" Basi sawa mpe pole sana mzee kesho nitakutumia fedha kidogo za matumizi nikuache sasa nataka nilale .. Usiku mwema mpenzi wangu" Alimalizia mwakibubu.

Baada ya kukata simu bwana mwakibubu alishikwa na hofu na kufikiri labda kuna nyeti mama amigo atakuwa kadokezwa au labda baba pachu kamwambia ukweli mamapachu na mama pachu kaamua ashirikishe mama amigo au labda chamdoli kampigia simu.

Alinyanyua simu yake na kumpigia baba pachu ambaye alipokea na alipojaribu kumhoji baba pachu alikataa na kugoma kuendelea kuongea kwa madai ya kuwa anaidumisha ndoa yake usiku huo ambayo hapa katikati ililegalega sana na kukubaliana waongee asubuhi yake.

**********************************************************************************************

Saa nne kasoro asubuhi bibi gusa unate alionekana akiwa kwenye ule uchochoro aliokutana na yule binti aliyemzawadia nyoya na kuondoka na fedha laki na nusu.

Akiwa pale anajisemesha semesha juu ya kumtafuta yule dada aliyempa nyoya mara sauti ya dada mmoja aliyekuwa pembeni alisogea na kuongea.

":wow wow wow kumbe ndio wewe yule bibi uliyempa dada mwalumbepa lile nyoya la bahati?

Nilikuwa nakutafuta sana bibi huwezi amini yaani leo nimekutana na wewe hakika Mungu sio athumani eeeh jamani bibi na mimi nilipe shilingi ngapi unisaidie?" alihoji huyo binti

Kwa haraka yenye uchu wa hela bibi gusa unate alitoka pale aliposimama na wale mabinti na kwenda upenuni mwa nyumba na kusema kwa sauti ya chini,

" Mjukuu wangu chamdoli kwa hili nisamehe tu, Give me only this one last chance nitengeneze hela ya mwisho" kisha akazima simu na kurudi huku akiwa kaokota jiwe moja laini sana akilipekecha mkononi.

"Mjukuu, wewe una roho kali sana na kila karipio lako watu wanakuogopa" aliongea bibi huku akilipekecha lile jiwe na kisha akamshikishaa mkononi lile jiwe yule binti na kumuuliza

" Umejisikiaje mjukuu?"

Yaani bibi kila nikipekecha hili jiwe mawazo yote yanahamia mkononi kwani lina nini? alihoji huyo dada

Bibi gusa unate akamwambia yule dada ": wewe una nyota ya parachichi, si unalijua parachichi?"

"Ndio bibi" alijibu dada

"Basi wewe unaweza kutumika kama chakula, tunda na juice kwa wakati mmoja na kumbuka hata kwenye fruit salad wewe huleta ladha zaidi kwa kila tunda utakayochanganya nalo na pia wanaokupatia hukula wakikuchanganya na chumvi kama tunda na sukari kwenye juisi unajua tafsiri yake?" Alihoji bibi

"Hapana bibi nisaidie hakika nimegundua kwa nini dada mwalumbepa anakufagilia unaongea kwa mifano isiyo rahisi kufahamika" alisisitiza huyo dada

" Mjukuu inamaana kuwa wewe una vipaji vingi sana na uwepo wako unakubalika kila sehemu na ni mtu wa mafanikio ila natakiwa kukuongezea ujasiri.

Hivyo hilo jiwe ni dawa kwani kila utakapotaka kufanya jambo ukilishika jiwe hilo na kujisemea mwenye kuwa nitaweza hakika ni dakika chache tuu utafanikiwa ila kamwe usilidharau hilo jiwe maana utaishia kwa mtu wa kishindwa kwa kila jambo."

Baada ya maneno hayo bibi akaongeza kwa lugha nyingine ambayo haikufahamka kwa haraka akisema, Kipompi!! pompi!!! kipompelee!! limpampa!! na baada ya kumaliza yule binti akauliza ni nini hicho umeongea?

Hiki ni kiyaudi mara ya mwisho niliongea wakati nimelitembelea kaburi la mtoto wa yakobo huko mashariki ya mbali na baada ya maneno haya mvua kubwa sana na wakazi wa kijiji kile walikinga sana madumu ya maji kuonesha ni mvua ya baraka.

Lakini leo baada ya maneno haya nafikiri mizimu ya TIKISA MDODO itakuwa imepokea dua hii hivyo sasa wewe weka hela mapema ubaoni nikaendelee kukusafishia nyota.

Shilingi ngapi bibi niweke ubaoni" alihoji binti

Mizimu haipokei zaidi ya laki na nusu ila kama unaweza kulipia kwa hela ya kwacha ya zambia mizimu yapokea pia.Haya namba yangu hiyo hapo na ukiwa unatuma imba Kipompi!! pompi!!! kipompelee!! limpampa!! na kisha utanirushia na namba ya dada yako mie niko ON DUTY bye.

Aliondoka bibi gusa unate na baada ya nusu saa aliwasha simu na kupokea ujumbe wa kuwa hela imeingia kiasi cha shilingi laki mbili pamoja na namba ya dada mwalumbepa na ujumbe kutoka kwa mtumaji ukisema,

" Hakika wewe ni bibi wa faraja na utaishi maisha marefu sana asante. Hiyo shilingi elfu hamsini ni zawadi yangu kwako na mizimu uipe hiyo laki na nusu tuu"

Bibi Gusa unate alicheka zadi na kusema ama hakika mjini shule kwanini nakuwa mzee ningeanza kampeni hii miaka ya nyuma hivi sasa ningekuwa namiliki mjengo wangu wa ukweli hapa mjini kisha akaanza kujongea kwenye kibanda cha kutolea fedha.

Akiwa kasimama anasubiri kupokea hela yake kutoka kwa muhudumu wa kibanda kile mara simu yake iliita...........

Je simu ilimtaka nini Bibi Gusa Unate?

Usikose kisa hiki leo jioni

MUHIMU

Neno kutoka kwa mdhamini

Gracious HOUSE of CAKES tunakukaribisha Forest ya zamani.. nyuma ya Green lounge pembeni ya Penge kwenye duka letu. utajipatia Cakes za kila aina. Magic popcorns na suprises cup cakes. tunapokea oda hata za mwakani sababu tanapenda kufurahi na wewe. tunaanda bday party kwajili ya watoto na hata watu wazima kwa bei nzuri tuu.. kaa hunanafasi yakuja pia usipate mawazo sababu tunakuletea utakacho mpaka ulipoo. KARIBUNII SAANAA.

KUMBUKA

Kama unataka kusoma visa vya mwanzo tafadhali tuma Simu ya Ajabukwenda whatsapp namba 0713317171

Share, like Simu ya Ajabu na comment ili kisa kingine kiwahi kuletwa

OMBI

Unaweza kuwa nawe mdhamini wa simulizi hii tamu kwa kuwasiliana nasi kwa kuandika neno UDHAMINI kwenda whatsapp namba 0713317171

You Might Also Like

0 comments: