Spaghetti zasambaratisha ndoa ya Daktari bingwa

14:55:00 Unknown 0 Comments

Daktari mmoja alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na nesi mmoja aliyekuwa akivutia sana katika hospitali yake.

Baada ya mahusiano yao kupamba moto hatimaye yule nesi akapata ujauzito na kumwambia yule daktari.

yule daktari akamwambia, "ukibaki hapa bongo wife akija kugundua ataweza hata kukukodia watu wakuangamize, sasa cha kufanya utaenda italy ukakae huko na kujifungulia huko."

Nesi akamwambia, "sasa utajuaje au nitakutumiaje taarifa kuwa nimejifungua?"

Daktari akasema si wajua mke wangu hajui kiingereza?, sasa wewe tutanitumia postcard na nyuma yake niandikie kwa kiingereza neno 'Spaghetti' na mimi nitajua umejifungua salama na nitakutumia fedha za matumizi.

Nesi akachukua feda za nauli na za kuanzia maisha kule kisha akasafiri kwenda majuu.

Miezi sita baadae mke wa dokta akiwa nyumbani akaletewa postcard yenye jina la mmewe na kumpigia daktari na kumwambia katumiwa postcard kubwa sana, dokta akamwambia atarudi na kuisoma baadae.

Jioni daktari aliporudi akaichukua ile postcard, baada ya kusoma akazimia pale pale na kukimbizwa hospitalini, mke wa daktari akawauliza wauguzi wakasema dokta kapatwa na mshtuko hivyo lazima apumzishwe kwanza pale hosptal.

Mkewe akarudi nyumbani na kuisoma ile postcard, akaona imeandikwa maneno ya kiingereza, "'Spaghetti, Spaghetti,Spaghetti, Spaghetti -Two with sausage and meat balls,two without.'"

You Might Also Like

0 comments: