HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " SEASON FINALE

22:08:00 Unknown 0 Comments



HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SEASON FINALE 

ILIPOISHIA JANA

Aliwaamsha na kuwasalimia na kwa uchovu wakaamka na baada ya kuamka akamvuta mwakibubu nje na kumpa mkasa mzima wa hospitali na juu ya ile simu ya chamdoli na hapo wakaanza kuliwasha gari kuelekea mjini waweke mafuta na kuanza kazi za kuwatafuta wale wageni wa jana yake jioni bila hata ya mwakibubu kujiandaa.

Walipotokezea barabara kuu ya kwenda mjini walishangaa kuona watu wengi wakiwa wamesimama wamelizingira gari moja na waliposimama na kulisogelea kundi hilo la watu baba pachu aliishiwa nguvu baada ya kuona ni ajali iliyotoa uhai wa watu na mmoja wao kati ya hao waliogongwa akiwa ni.............

MWENDELEZO

Walipotokezea barabara kuu ya kwenda mjini walishangaa kuona watu wengi wakiwa wamesimama wamelizingira gari moja na waliposimama na kulisogelea kundi hilo la watu baba pachu aliishiwa nguvu baada ya kuona ni ajali iliyotoa uhai wa watu na mmoja wao kati ya hao waliogongwa akiwa ni mzee tobo bao.

Baba pachu aliikumbuka vizuri ile sura na alipoangalia kwa ukaribu akagundua hata yule aliyefuatana naye jana yake jioni nae alikuwa amefariki akiwa pamoja na kijina mwingine aliyetambulika kuwa ni dereva bodaboda.

Baada ya kupeleleza aliambiwa walikuwa wamepanda kwenye bodaboda moja wakiwa watatu maarufu kama mshkaki ili wawahi gari la kwenda kijijini kwao wakitokea nyumba ya kulala wageni.

Baba pachu hakuongea neno lakini uso wake ulionesha kila dalili ya yeye kuchanganyikiwa na kuanza kujisemesha, " duuh, sasa mbona mambo haya yanazidi kuniwia magumu na ushahidi huu nitaupata wapi? shahidi namba moja ndio huyo kashatututoka" alijisemesha baba pachu huku akiliendea gari lake na kisha wakaondoka na mwakibubu.

Waliondoka na gari lile na kutembea umbali mrefu bila hata ya kujua wapi wanaelekea mpaka pale baba pachu alipolisimamisha gari kwa kasi

" kaka vipi sasa huku unakoelekea ni wapi?"

" mwakibubu nimechanganyikiwa sana hapa na sijui nini kinataka kututokea katika maisha haya"

" kaka mimi naona tukalewe tuu muda huu maana kichwa changu hakiko sawa na jana nimelala na familia nzima pale sebuleni"

" sasa kaka masihara hayo wewe unafikiria kulewa tuu na shingo lako bovu hilo???"

"Ndio dawa yenyewe maana tunazidi kupoteza uelekeo na hata zile dawa hazijanitoka kabisa mwilini mwangu sijui niende wakanipe nusu kaputi tena nilale na niamke mapema mwakani yaani huu mwaka naona ni washetani hata temba aliwahi kuimba ingawasikumtilia maanani"

" kaka dawa ya matatizo sio kulewa kwani tangu chamdoli atokee tumelewa zaidi ya mara mia na hakuna suluhu zaidi ya vioja na majanga, mimi nakushauri turudi nyumbani wewe kamcheki mama amigo maana anaweza kukuliwaza na mie nikaongee kidogo na pachu si wajua nimemwacha muda mrefu sasa na leo nilimkataza asiende shuleni... wewe nitakupigia baadae, ngoja nikupeleke nyumbani"

" hapana baba pachu wewe niache hapa nipitie kwa mangi hapo nichukue mahitaji kidogo"

" poa basi nitakupigia baadae" alimalizia baba pachu huku akiwasha gari na kuondoka eneo hilo akielekea nyumbani.

Ilikuwa ni mida ya saa nne na nusu za asubuhi nesi mwalikumba alionekana akitembea mwendo shari akielekea sehemu alikofikia bibi gusa unate.

Alipofika pale mapokezi aliomba aitiwe bibi haraka na baada ya dakika kama 20 za kumsubiri hatimaye bibi alionekana akija huku akiwa hoi kwa vyombo vya jana yake jioni

" Tsup Men..... mambo nigaje ? mbona tunamaliziana stimu za usingizi mzazi?"

" Tafadhali bibi naomba uache kunisemesha lugha zako za kihuni, nimekuja hapa kwa jambo la muhimu naomba tukae sehemu tujalideli" aliongea nesi mwalikumba huku akitafuta sehemu ya kukaa na kuanza kuongea

" ndugu yangu, jana uliona ile simu aliyopigiwa mama pachu na kuzimia??? nimeifikiria usiku kucha nimeona kunauwezekano wa kila mtu kupigiwa na kuzimia kwa aina ile"

" hapo umenena, kwani wewe ushapigia simu hivi karibuni na huyu chamdoli"

"hapana bibi"

" sasa hapa hatutakiwi kumwongelea tena kama mtu hujapigiwa ni bahati yako na unatakiwa uondoke kimya kimya au sio nesi?"

" mmh ni kweli ila yule hatabiriki bibi" aliongea nesi mwalikumba na ghalfa meseji iliingia kwenye simu yake na alipoifungua na kuisoma aliondoka kwa haraka bila hata ya kumwaga bibi huku akipiga mayowe.

" heee mamaaa inamaana huyu chamdoli meseji zake zina pilipili? au nesi katumiwa meseji na wanaomdai pango la nyumba maana hapa mjini ni mipango"

Bibi alikaa pale kwa dakika kama sita akimcheka nesi mwalikumba kwa kuikimbia meseji kabla ya yeye kutumiwa ujumbe uliomfanya asimame haraka bila ya kutafakari na kuingia chumbani kwa mendo wa haraka na kuondoka na begi lake dogo bila hata kuaga na kuonekana akielekea kituo kidogo cha mabasi huku viatu akiwa kavisika mkononi.

Mama pachu alikuwa kaishika sigara yake huku akiwa anaitazama simu yake iliyokuwa ikiita na mpigaji akiwa ni baba pachu bila hata ya kushtuka na kuendelea kuivuta sigara yake huku akishushia na bia yake na dakika mbili baadae alionekana akiwa anajisemesha peke yake maneno ambayo hayakusikika huku akikizunguka chumba chake kama mtu aliyewehuyuka.

Akiwa bado yuko katika tafakari nzito iliingia meseji nyingine iliyosisitiza kwa kusema " Hebu jaribu kuufikiria uhai wako kwanza, maana naona kama hujitambui.... nimekuambia anza safari sasa, usizijaribu hasira zangu"

Mama pachu alisimama na kuanza kuondoka kwa haraka akiwa kavaa miwani yake nyeusi ya jua na kofia iliyofumwa kwa mkono na kumfanya asitambulike kirahisi na kuanza kutoka pale na dakika chake alioneka akiwa amepanda nyuma ya bodaboda akielekea kusikojulikana.

Saa saba kamili za mchana baba pachu na mwakibubu walikutana pamoja hodari hotel ili wapate chakula cha mchana kwa pamoja baada ya baba pachu kuzunguka huku na kule akimsaka mama pachu bila mafanikio na cha zaidi ni baada ya kuonana na munu ambaye aligoma kuongena neno lolote na hatimaye kumkimbia baba pachu.

Baada ya kusimuliana na mwakibubu juu ya ripoti hiyo walianza kula huku mwakibubu akionesha jinsi ambavyo ameshayachoka maisha kwani ndoto zote kazifukia na anahisi kuwa muda wowote anaweza kufa na hata kuipoteza furaha ya familia yake ambayo sasa imekuwa haieleweki.

Ni wakati huu ambapo mwakibubu alikuwa akiendelea kumsimulia zaidi baba pachu ndipo akapata mshangao wa mwaka baada ya baba pachu kuipokea meseji kwenye simu iliyomfanya anyanyuke bila hata ya kuangana na mwakibubu na kuanza kuondoka na gari lake kwa kasi akelekea kusikojulikana.

Mwakibubu alishangaa kwa muda akiwa pale na kuamua kuondoka baada ya kumpigia baba pachu bila mafanikio ili kujua nini kimemsibu na hatimaye akarejea nyumbani kwake na kuanza kucheza na watoto wake akiwa na hofu kubwa juu ya swahiba wake baba pachu ingawa akaamini kuwa lazima angerudi na kumpa taarifa.

Wakati huo mama amigo yeye alikuwa busy akimwangilia mmewe aliyekuwa akicheza na watoto kwa furaha kabla ya kumshuhudia akichanganyikiwa na kutoka nje haraka bila hata ya kuaga na kuwasha gari na kuanza kuondoka jambo lililompa wasiwasi mama amigo naye akaanza kumfuatilia taratibu huku akimtumia meseji jirani ili amsaidie kuwaangalia watoto na baada ya dakika kumi naye alikuwa ndani ya tax akimfuatilia kwa ukaribu mwakibubu ambaye alianza kuucha mji.

Saa tisa kasorobo gari moja dogo lilionekana likija kwa kasi na ................

" ASANTE SANA MPENZI MSOMAJI WETU KWA KUIFUATILIA SIMULIZI HII MPAKA LEO AMBAPO INAFIKIA UKINGONI KWA UPANDE WA FACEBOOK ILA KITABU CHAKE KITAKUWA MKONONI MWAKO TAREHE 1/12/2014 NA UTAMALIZA MKASA HUU AMBAPO UKWELI UNAELEKEA KUONEKA NA CHAMDOLI KUFAHAMIKA ILI KUPATA NAKALA YAKO AU KUWA WAKALA WASILIANA NASI KWA NAMBA 0713317171 NA EMAIL FRED@SMARTIDEAS.CO.TZ".

Karibuni katika ukurasa mama kuendelea kusoma visa vingine ..... ukura unaitwaTabasamu na Fuledi

You Might Also Like

0 comments: