ISHI KWA KUAMINI NA SIO KWA KUONA

16:52:00 Unknown 0 Comments



Imani ni kuamini vile ambavyo hauvioni na malipo ya imani ni kuona vile unavyoviamini.


Kwa yule ambaye ana imani hakuna ufafanuzi unaohitajika kwake kwa jambo lolote lakini kwa yule ambaye hana imani hakuna ufafanuzi unaweza kueleweka kwake.


Imani inategemea zaidi uwezo wa mtu kuamini hata kama vitu viko nje ya upeo wa kawaida wa kuamini mambo

Maana tunaishi kwa imani, na si kwa kuona

2 Wakorintho 5:7

Kuwa na imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayotumainia; kusadiki kabisa mambo tusiyoyaona.

Waebrania 11:1

Sio sisi tuu ndio wa kwanza katika kukumbushwa kuhusu kuwa na imani ya kile tukiaminicho bali hata wazee wa kale walipata baraka kwa imani

Maana wazee wa kale walipata kibali cha Mungu kwa sababu ya imani yao.

Waebrania 11:2

Hivyo basi


1.  Sasa imani ni kuwa na uhakika kwa kile tunachokitegemea na hatukioni kwa macho.

2. Mababu zetu wa kale walitumia imani kuamini na wengi walibarikiwa ba hata kuongea na Mungu moja kwa moja ikiwa ni pamoja na kukamilisha majukumu waliyopewa na  mfano wao ni kama vile MUSA, ABRAHAM aliyekuja kupewa jina la baba wa imani na wengine wengi.

3 Kwa imani sisi tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hivyo tukionacho sasa hakikuumbwa kwa kutokana na kile kilichokuwepo wakati huo. 

4 Kwa imani Abeli ​​alimtolea Mungu sadaka bora zaidi kuliko Kaini. Kwa imani alikubaliwa kuwa mtu mwenye haki, Mungu alizungumza vizuri kuhusu sadaka zake. Na kwa imani yake bado anaongelewa  ingawa amekufa.

Kwa imani Henoki alichukuliwa kutoka maisha haya ili asife kifo cha kawaida na hakuweza kupatikana kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua. Awali kabla ya alichukuliwa alikuwa ni mtu aliyempendeza Mungu kwa matendo yake.
Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa sababu mtu yeyote ambaye hutaka kumpendeza Mungu ni lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta kwa bidii.
Kwa imani wakati Nuhu alipoonywa kuhusu mambo yasiyoonekana akajawa na hofu takatifu na akajenga safina kuokoa familia yake. Mungu aliuhukumu ulimwengu na Nuhu akawa mrithi wa haki kwakuwa alikuwa na imani.
Kwa imani Abraham alimtii Mungu alipoitwa kwenda mahali baadae kupokea kama urithi wake, alitii na aliondoka akaenda ingawa hakujua aendako.
Kwa imani aliishi nyumbani kwake katika nchi ya ahadi kama mgeni katika nchi za kigeni; aliishi katika mahema pamoja na Isaki na Yakobo ambao pia walikuwa warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
10 Maana kwa imani alikuwa akitazamia mji wenye misingi ambao umebuniwa na kujengwa na Mungu.
Tuna mifano mingi sana kuhusu watu waliokuwa na imani na wakatimiziwa mahitaji yao na kama haitoshi tunaishi katika dunia na familia zetu tukishuhudia kila siku miujiza ikitendeka kwetu au kwa wenzetu hasa tunapokuwa na imani juu ya jambo fulani

Wewe una amini na una imani juu ya kile usichokiona ili kitokee?

Mfano unafiria kuwa na maisha mazuri ambayo hauyaoni je una weka imani yako na kuhakikisha unaamini katika kufanikiwa?

KuMBUKA

Mungu amekupangia kitu kizuri maishani mwako unachotakiwa ni kuanzia sasa kuwa na imani ya kile ukifanyacho na kuamini Mungu atakibariki na kukifanya kionekane

You Might Also Like

0 comments: