Kamwe usikubali kuota ndoto kama hjii

22:48:00 Unknown 0 Comments

Ilikuwa ni jioni moja baada ya kumaliza kazi zangu niliamua kwenda katika hotel moja maarufu hapa jijini Mbeya ili kupumzika nikipata vinywaji pamoja na kuongea na jamaa zangu huku tukipata nafasi ya kubadilishana mawazo yenye lengo la kuboresha kazi zetu.

Kwa kawaida huwa sipendi sana kukaa sehemu za starehe mpaka mida mibovu kwani huwa napenda kuwahi kurudi nyumbani na kupata muda wa kuchati na kucheza na watoto pamoja na mama yao na kamwe sikutaka chakula cha usiku nile nje ya nyumba yangu au kula huku watoto na mama yao wameshakula.

Basi ilipofika mida ya saa tatu kasoro niliagana na marafiki na kisha nikatoka zangu nje  ili nianze safari ya kurudi nyumbani. Nilipofika pale nje nilikopaki gari langu nilimkuta dada mmoja aliyekuwa kaegemea gari langu akilia kwa uchungu mkubwa.

Nilisimama pale kwa zaidi ya dakika moja bila kumwambia kitu chochote na baada ya uzalendo kunishida pamoja na muda kunitupa mkono nilimsogelea dada na kumsalimia ingawa hakuniju nikamwomba asogee pembeni ili niondoke na gari langu.

Mbaya zaidi ni kwamba binti aliendelea kulia bila kuonesha dalili ya kunisikiliza na wakati huu nikawa mkali kidogo na kumwomba anipishe, lakini dada ailinuka na kuniangalia usoni na kusema " naomba kaka uniache kwa muda nipumzike, nitakupisha kwani nina wakati mbaya sana hapa"

Kweli nilimpisha na kurudi ndani mara moja na kumvuta rafiki yangu mmoja aitwaye bwana Shukurubu na kumwambia yaliyonisibu nje. Alinisihi kuwa ni vyema niende na kumhoji ana matatizo gani yaweza kuwa masuala mapenzi si wajua vibuti vinavyotawala siku hizi?

Basi nikatoka mpaka pale nje na kwa upole nikamuuliza ni yapi yaliyomsibu muda huu wa usiku kama huu. Huku akitokwa na machozi yaliyoambatana na kilio cha kwikwi dada alianza kunisimulia kwa kusema, 

" kaka yangu mimi nimechumbiwa na kijana mmoja ambaye tulifahamiana naye miaka michache iliyopita, na tukaanza taratibu zote za harusi na hivi juzi ilikuwa iwe send-off yangu na amekuwa hapatikani na nilivyojaribu kumtafuta nikashindwa zaidiya kusafiri kutoka Dar na kuja hapa.

 Nimefanikiwa kuonana naye ila jibu alilonipa na nilichokishuhudia kwa macho yangu kimeniumiza sana kwani muda wote huo kumbe alikuwa ananitumia kwa kuwa niliachiwa mali nyingi na marehemu baba yangu na alitaka kuja kunitelekeza kabla ya mkewe wa ndoa kumshtukia .....

 kaka nimeumizwa sana na sijui nifanyeje hapa nilipo kwani sina hata sent ya kunirudisha dar wala ya kunipatia malazi   usiku huu"  alimaliza kuingea binti huyo huku akiangua kilio cha uchungu kilichonipelekea na mimi kulengwa na machozi.

Kiukweli nilichukua waleti yangu na kutoa noti ya shilingi elfu kumi na nilipotaka kumpa wazo likanijia kuwa alihitaji msaada zaidi hivyo nikajivuta mpaka nyuma ya hoteli na kumpigia mke wangu kumweleza hali halisi ya huyu binti na akakubaliana na mimi kuwa anahitaji msaada hivyo nirudi nae nyumbani na siku ya pili tumfanyie utaratibu wa kurudi Dar.

Tuliondoka pale na kufika nyumbani ambako mke wangu alitupokea na baada ya dakika chache familia nzima ikawa mezani kwa chakula cha usiku. Tuliendelea na mzungumzo huku akitusimulia juu ya safari yake na majanga yaliyomsibu na wote tuliishia kumhuzunika na kumpa pole na kisha muda mfupi baadae alionesha sehemu ya kupumzika na wote tukaenda kukalala.

Asubuhi nikiwa katika maandalizi ya kuondoka mlango wa chumbani kwetu uligongwa na haraka mke wangu akajibu karibu akijua ni mtoto wetu ambaye alikuwa na kawaida ya kutuaga kabla ya kwenda shuleni. 

Mke wangu aliyekuwa amelala aliamka na kwenda kuufungua mlango lakini cha ajabu na cha kushangaza yule dada aliingia moja kwa moja mpaka chumbani na kuanza kupiga kelele akisema,

 " Yaani nimekuvumilia nimeshindwa ulidai nidanganye kuwa mimi nina matatizo, na kuwa usiku ungemkimbia mkeo na kuja chumbani kwakungu tulale wote lakini umepitiliza mpaka sassa, unaniona mimi kinyago wako? kama ni hivyo kwanini uliniita toka dar na kwa nini leo hukunipangia hoteli kama kila siku unavyofanyaga?"  

Hakika niliishiwa nguvu na sikuweza kuongea kitu na kumwangalia mkwe wangu ambaye wakati huo naye alikuwa hajui acheke, alie kwa sauti au anipige nikiwa siju nini nifanye yule binti alikomelea msumari wa mwisho kwa kusema.

"kwanza ulisema hii yumba ni ya mwanangu People sasa kwa nini hizo document huni au nianze uchizi humu ndani???? Nauliza!! na kama hutaki kumwambia ukweli mkeo leo moto utawaka hapa ndani na siendi popote nimechoka kukaa WInome Guest kwanza chafu na ni kama unanidhalilisha"

Nilinyanyuka na kumzaba kibao kmoja na wakati nikiwa natafakari nini kifanyike nilishangaa kuona mke wangu akipaki vitu vyake na kama haitoshi akaufunga mlango kwa nje na kuondoka.

Wakati huu machozi yalianza kunitiririka na kujisuta kwa wema wangu nilioufanya na kuamua kumpigia rafiki yangu tuliyekuwa wote jana usiku na kumpa mkasa mzima. Alifika pale na kutufungulia mle ndani na hapo sasa nilimchapa yule binti na akatoka mbio bila kujua wapi alielekea.

Tukaanza safari ya kumtafuta mke wangu ambaye ilionekana kuwa hajaenda mbali kwani kila kitu chake kilikuwa nje na baada ya muda mfupi wa kumtafuta nilifanikiwa kumkuta nje kidogo ya shamba letu la ndizi akiwa anahema kwa taabu na mapovu yakimtoka. Kwa haraka nilimbeba na kuanz akukimbia naye ambapo hata kabla ya kufika hospitali alinifia mikononi mwangu.

Nililia kwa uchungu mkubwa nikiomba msaada na hata kabla sijasikiwa kilio changu mara polisi walikuja wakiwa na yule binti akiwa na wenzake wanne na mtoto mdogo na kunirushia wakidai kuwa ni mtoto wangu.

Nikiwa sijui hata nimshikaje huyo mtoto nisiyemfahamu mara polisi wakagundua kuwa mke wangu amekufa hivyo wakanichukua pamoja na maiti mke wangu ambaye kwa sasa ni marehemu na kunipeleka kituoni baada ya mke wangu kuwekwa mochwari.

Nilianza kulia nikiwaita watoto wangu huku nikijiuliza ni shida gani niliyomkosea Mungu mpaka kuniacha nikiwa hivi. Wakati naendelea kutafakari kwa uchungu nikiwa pale polisi alipita kwa mbali bwana Sankoma Fuledi ambaye alikuwa ni mpinzani wangu katika biashara na aliyesema kuwa angeipoteza furaha yangu na ndoto zangu kwa kuwa nilifanikiwa kumshinda katika tenda moja ya kusambaza vitabu ya mashukeni akiwa ananicheka na kunipa alama ya dole gumba kama vile ishara ya kushinda vita.

Nililia kwa uchungu sana lakini kilio kile kilizimwa na kirungu kimoja kilichopigwa kichwani toka kwa afanye mmoja akinitaka nitulie kwani nilikuwa nasumbua wenzangu kilirungu hicho kilinifanya nishtuke usingizini muda huu na kugundua ilikuwa ni ndoto na hakuna ukweli wowote 

Kuangalia pembeni nashuhudia me wangu akiwa kalala usingizi wa fofofo.... duuuh haki ya nani tena hii ndoto ni mbaya 

 

You Might Also Like

0 comments: