"Kamwe usithubutu mwanamke akuvulie pete ya ndoa"

22:54:00 Unknown 0 Comments


Msemo huu marehemu mzee wangu alipenda sana kuutumia na mara kwa mara alinisisitiza kuwa kama nitaona bado muda wa kuoa haujafika nitulie kuliko kuingia kwenye mahusiano huku nikiwa macho juu juu.
Kiukweli msemo ulie niliuchukulia kianalojia sana na kuona ni jinsi gani mzee alitaka kunitishia kuhusu maisha ya mahusiano na kunifanya niwe mme bwege.
Nikawaza kama nitakuwa naogopa hivyo si kuna siku wife atanipa kazi ya kumpikia na kumnyenyekea kitu ambacho enzi hizo mie na jamaa zangu tulikishangaa sana hasa kwa kuwa na jirani yetu ambaye yeye alichota maji na kumpikia mkewe na watoto pia.
Kwa utafiti wa vijiweni tukagundua jamaa alipewa kitu cha songea maarufu kama limbwata na hata tulipokaa nae kijiweni hatukumpa nafasi ya kuongea tukamkubali kwani tulihisi sio dume la pointi.
Miaka michache baada ya kuhitimu chuo nilibahatika kuoa ingawa naumia kuwa marehemu mzee wangu hakuwepo ila niliamini kiroho yupo nami hata kama kimwili hayupo nami.
Binti huyu nilikutana naye mara ya kwanza kwenye usaili wa kazi pale Smart Ideas na kiukweli nilimpenda ghafla ingwa nilishindwa kupata mawasiliano yake mpaka naondola pale.
Nikajaribu kumsaka facebook kwani miaka ya 2008 fb ndio ilikuwa ishaanza kuwa maarufu kwetu sie wanaume walafi wa mabinti lakini huyo binti hakuwepo basi niakamia na kusahau.
Wiki nne baadae nikapigiwa simu na ile kampuni kuwa wilihitaji watu wawili pale ofisini na mmoja kashindwa kwenda hivyo mie niliwekwa kuwa wa akiba hivyo kama bado sijapata kazi niende.
Kwangu ilikuwa ni zaidi ya zali na kwa furaha niliyokuwa nayo ilinibidi nivute pumzi ndefu iliyoambatana na mwendo wa haraka mapaka bar ya jirani na kuagiza kinywaji kikali.
Niliwahi kufika zangu ofisini jumatatu ile hasa ukizingatia siku ya kwanza hivyo nilihitaji kuwa mwenyeji na mazingira ya pale na nikapiliza kantini kupata supu.
Macho yangu yakagongana live na Salome yule binti ambaye nilimpenda ghafla siku ya usaili kumbe sie wawili ndio tumepata bahati ya kazi pale tena mie kwa bahati bahati maana kama yule mnaa mwenye nafasi yake angekuja mie ningeambulia patupu.
Ilinichukua miezi mnne Salome akanikubali na kwa chini chini tukawa wapenzi. Mapenzi yakakua na kuwa matamu zaidi ya kusoma na kukomenti baadhi ya post zako wewe uisomaye hii story hapa facebook.
Salome anakuja kupata akili sawa sawa ilikuwa ni mwaka mmoja na nusu tuko kwenye mahusiano, ana mimba changa, tunakaribia kufunga harusi na siku hiyo ndio namvisha pete ya uchumba mbele ya marafiki zake na baadhi ya ndugu jamaa na marafiki.
Kuna kipindi nilishikwa na hasira, kuwa mkali, kuwa mbinafsi na hata asilimia za wivu kupanda kwa jinsi watu walivyomkodolea mimacho na hata walivyomsumbua kuwa nao lakini yeye akawa na msimamo.
Binti ambaye kama mwanaume angepishana nae na asigeuke kimwangalia, kumsemesha, kujichekelesh na hata kuomba namba basi huyo mwanaume angefaa apelekwe kwenye maombi maana ana pepo kali sana la kiburi.... Kiufupi alijaliwa uzuri na msimamo.
Miaka mitatu baada ya harusi mie nikawa nimefanikiwa kufungua kampuni ya familia na kuisimamia huku yeye akiendelea na kazi pale ofisini kwetu kwa zamani.
Kesi za kufumwa na wanawake, kudakwa sms za kina dada kwenye simu yangu zikawa ni kawaida na nilipogundua kuwa simu anipatia nikaanza kuwa mtumiaji wa facebook.
Shukrani kwa bwana Mark kwa kutuletea facebook maana kila binti hata kama mtaani hakupendi ila ukipata akaunti yake ya facebook huwa hawana neno zaidi ya kukubali.
Matukio yangu yalizidi na hata muda wa kukaa na watoto wetu ikawa haupo tena. Alivyokuwa jasiri alikaa na mimi kunionya ikashindikana, akatumia wasimamizi wa ndoa, marafiki, baadhi ya ndugu lakini mie nikawa sasa kama nimelogwa.
Siku moja asubuhi aliniita na kuniomba nimsindikize hospitali lakini nikakataa nikaondoka na kwenda mishemishe. Narudi saa saba usiku nikashangaa kuona kakaa pale pale nilipomwacha asubuhi akiwa hajagusa kitu...
Moyoni nikaanza kuumia hasa baada ya kuona yeye na watoto wakiwa macho yamewavimba kwa vilio vya chini chini kwa siku nzima.
Nikajikaza na kumwambia una tatizo gani lakini hakujibu akazidi kulia mimi nikalala zangu. Asubuhi naamka yuko pale pale kakaa.
Duuh, unajua hii ilinifanya nishtuke na mbaya zaidi alikuwa akiniangalia tu bila kuongea lolote.
Chumba kikaanza kuwa chamoto na kama haitoshi moyo ule wa utu ukaanza kurudi nikanyanyuka na kwenda jikoni nikaandaa kifungua kinywa nikaja na kumwita ale.
Alikuja mezani na kukaa kwa sekunde kadhaa akitazama chini na kuniambia, " its too late Dan" kisha akaivua pete yake na kunikabidhi.
"Nimekuvumilia kwa zaidi ya muaka mitatu ya kudharauliwa, kutopewa thamani yangu na hata kutochambua mchango wangu ambao nimeutoa kwako mapaka leo unagombaniwa na kila mwanamke na kuosahau familia yako hasa wanao......WE DONE" alimalizia Salome.
Jitihada za mtuliza hazikufua dafu nikaona niondoke kama kawaida na kwenda zangu kazini na nikirudi atakuwa katulia nimwombe yaishe kwani maneno yale kweli hata kama ni kiburi yaliniingia.
Nilirudi toka kazini saa moja na nusu usiku na kuona hakuna dalili za watu mle ndani nikaingia chumbani na kuona katoa kila kitu chake na watoto na pete ile ya ndoa kaiweka juu ya kitanda.
Simu zote hazipatikani nikajaribu kuwapigia baadhi ya marafiki zake na baadhi ya ndugu ila hakuna aliyeonyesha kufahamu salome aliko.
Nikaenda kuripoti polisi na usiku ule sikulala mpaka asubuhi bado ikawa kimya. Ofisini siku ya pili yake nilipoenda kuwauliza wakanishangaa kwani salome alishaacha kazi mwezi mmoja uliopita.Nikaanza kuhisi kuna kitu salome kaaamua.
Miezi ikapita salome hayupo wala taarifa zake huku ndugu wakiniandama nami nikizidi kukonda kwa mawazo na biashara zangu kudorora kila kukicha.
Nikaachana na pombe pamoja na starehe nyingine lakini bado nikawa nazidi kutetereka kwenye biashara huku mikopo bank nikishindwa kulipa.
Kanisani sikupungua na nikimwomba Mungu japo anipe nafasi ya kumwona mke wangu nimwombe anisamehe na anitolee laana iliyokuwa mbele yangu.
Hali ikazidi kuwa mbaya nyumba ofisi nikaifunga kwa kukosa huduma na pango magari nukauza ili niweze lipa mkopo wa bank ambao nilikuwa na daiwa.
Marafiki wakapotea na hata pale nilipotamani kumpigia rafiki yangu yoyote kumpa salamu tuu jibu lao la kwanza lilikuwa, " kaka maisha magumu na hela haiparikani kabisa yaani"
Niliishia kukata simu kwa kuwa niliona kama ningeendelea kuongea nilikuwa najipalia mkaaa wa maumivu moyoni mwangu.
Ilafika kipindi hata uwezo wa chakula ukawa shida na hata nilipojaribu kuomba kazi ikaniwia vigumu kabla ya kuanza kuugua.
Nilianza kupatwa na maumivu ya kibofu cha mkojo na baada ya kunifanyia uchunguzi wakanifanyia upasuaji katika hospitali moja ndogo.
Upasuaji ule haukwenda salama nikapatwa na tatizo zaidi na sasa nikawa ninatoa harufu kali kiasi cha kuanza kukimbiwa na kila rafiki hata mtu wa kuniona.
Hakuna siku niliyoumia kama siku nilipomfuata rafiki yangu na kaka yangu mmoja anisaidie fedha na akaanza kutema mate na kunifukuza. Hakika nililia sana sana.
Siku moja nikiwa nimejifungia chumbani mlango ukagongwa sikuitikia maana nilijua atakuwa ni morgan yule muuza chipsi anakuja kuniletea chipsi kwani ndio pekee aliyenihurumia na kunusaidia kipindi hiki na alifanya hivyo kisa niliwahi kumwazima 10,000 wakati mama yake alipolazwa kijijini kwao.
Alifungua mlango binti mmoja na akaniuliza kama naitwa Dan, nikamjibu ndio, akaniambia nilitakiwa kwenda ustawi wa jamii kwani kuna mabinti watatu wametoa malalamiko yao juu yangu kwa kutowatunza wanangu.
Nikaanza kutokwa na machozi na kushindwa kujizuia kulia kwa sauti kubwa. Baada ya kumaliza kulia nikamuuliza dada, " je naweza kuja baada ya matibabu?"
Hapana tutakutibu kwanza na baadae shauri lako litasikilizwa, aliongea binti yule akinisaidia kunyanyuka.
Alinichukua na kunipeleka katika hospitali nzuri na ya gharama na wiki moja baadae nikaruhusiwa kupona na kupewa mapumziko ya siku kumi kabla ya kwenda ustawi wa jamii kusikikiza shauri langu.
Hofu yangu ilikuwa nitalipa nini nikiambiwa kulipa angalau salome mke wangu angekuwa hakuondoka na hati ya nyumba ningeuza na kukamilisha kila nidaiwacho na kuuhama mkoa.
Siku ya kwenda ustawi yule dada akaja kunichukua na moja kwa moja mpaka hotel moja na kuomba tule kwanza maana alikuwa hajala kisha tutaendelea na safari ya kwenda ustawi.
Nikashangaa kuona binti wa aina hii na ustawi wamebadika mpaka wanatoa huduma hizi?????
Nikiwa sijui kinchoendelea nikasilkia sauti za watoto wakiniita baba baba ile na geuka nakutana uso kwa uso na salome mke wangu.
Nikajikaza na kusimama wima ili nimwangalie vizuri, sikuwa na ujanja zaidi ya kumuuliza? Ni wewe uliyenilipia gharama za hospitali???? Akasema ndio na huyo ni rafiki yangu nilimwomba afanye hivyo ili upone.
Nikamuuliza tena je umerudi tuishi wote? Na ulikuwa wapi? Nilikumisi salome na wewe?
Akajibu tu kazi yangu ilikuwa kukuonyesha kuwa mimi ndio rafiki wa kweli na kwa kuwa umepona na umewaona wanao naondoka tena.......
Nguvu ziliniishia na kujikuta nashindwa kuuhimili mwili wangu nikasikia sauti ya simu yangu ikidondoka chini kabla ya kushtuka sasa na kugundua ni ndoto....
Nimehakikisha nikaona pete yangu iko mkononi sasa nimeanza Kufuta michepuko ya facebook maana yaweza kunifanya nivuliwe pete ya ndoa bure.....
Nakutakia siku njema..... Kama umeielewa ruksa kushare

You Might Also Like

0 comments: