Post chafu kuliko zote mtandaoni

16:46:00 Unknown 0 Comments

Lazima tukubali kuwa hapa duniani kuna watu wamezaliwa kuja kuwa watu muhimu katika jamii zetu hata kama tutatumia nguvu gani kuwafanya wasiwe hivyo.

Baadhi ya njia hizo tutumiazo kuwafanya wasifikie malengo yao huwa zenye makali na maumivu ya aina yake kwa wahusika.

Ila nimejifunza kuwa ni njia hizo hizo ambazo huwa ndio njia za kuwafanya watu hao wafikie ahadi zao.
Hebu chukulia kwenye maandiko matakatifu kupitia mfano wa Yusuph ambaye ndugu wakaamua kumuuza kabisa ili kumpoteza lakini kumbe ilikuwa njia ya yeye kuja kuwa mfalme.

Au angalia maisha yako na fikiri ni mara ngapi ulipitia mambo mazito na ya kutatanisha na mwisho wa siku ukafikia kufurahia ?

Zamani niliumia sana kuona kijana wa miaka 24 ana mafanikio wakati mimi nakazana na mipango isiyofanikiwa lakini nimekuja kugundua idadi kubwa ya watu huanza kuona mafanikio katika miaka ya 30 na.

Nikagundua kuwa unapoutumia vyema umri huo mdogo kujifunza kuhangaika na kuumia mara nyingi ukitetea mipango yako ndivyo unavyojipa nafasi ya umri huu kuvuna mafanikio.

Kila barabara uipitayo sasa ina maana kubwa na somo ndani yake miaka ya usoni.

Hebu itumie siku ya leo kufanya jambo litakalokuja kuwa faida siku za usoni.

Pia kumbuka hakuna hali mbaya ya sasa au mambo mabaya upitiayo yasiyo na maana katika maisha yako ya baadae.

Kitu cha msingi usife moyo na hali hizo zaidi ya kuwa na mtizamo wa kufanikiwa
Siku njema

You Might Also Like

0 comments: