CBE YATOA MSAADA WA MASHUKA HOSPITALI YA WAZAZI META

15:20:00 Unknown 0 Comments

(TZS)BURE

CBE YATOA MSAADA WA MASHUKA HOSPITALI YA WAZAZI META

CBE YATOA MSAADA WA MASHUKA HOSPITALI YA WAZAZI META - Image 1CBE YATOA MSAADA WA MASHUKA HOSPITALI YA WAZAZI META - Image 2CBE YATOA MSAADA WA MASHUKA HOSPITALI YA WAZAZI META - Image 3CBE YATOA MSAADA WA MASHUKA HOSPITALI YA WAZAZI META - Image 4CBE YATOA MSAADA WA MASHUKA HOSPITALI YA WAZAZI META - Image 5


Description

PROFMSAADADR

CHUO cha Elimu ya Biashara(CBE) tawi la Mbeya kimetoa msaada wa mashuka katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kitengo cha Wazazi Meta ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Emmanuel Mjema, alisema msaada huo unagharimu shilingi Milioni tano ikiwa ni sehemu ya kushiriki huduma za kijamii katika maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho
Alisema Chuo hicho kilianzishwa Januari 21, 1965 hivyo hadi sasa kimetimiza miaka 50 ambapo Chuo kinaadhimisha mafanikio hayo kwa kushiriki huduma za jamii kama mchango wake katika jamii ambapo mbali na kutoa msaada wa mashuka katika hospitali ya Wazazi Meta pia jumamosi ya wiki iliyopita walitembelea Hospitali ya Mkuranga.
Alizitaja shughuli zingine kuwa ni kutoa elimu ya ujasiliamali kwa vijana wa Mkoa wa Dar es salaam,Dodoma,Mbeya na mikoa mingine na kutoa elimu kwa wanaojiandaa kustaafu ili wawe na maandalizi ya kukabiliana na maisha baada ya kustaafu.
Mbali na msaada huo, Profesa Mjema alitoa wito kwa wafanyabiashara nchini kujenga utamaduni wa kuhudhuria masomo ya ujasiliamali ili waweze kufanya biashara zenye uhakika kwa kuweza kukokotoa faida na hasara tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi wao hufanya biashara kwa mazoea.
Alisema Vyuo vya CBE vinatoa nafasi za masomo ya jioni ambayo yatamwezesha mfanyabiashara yeyote kuweza kujiendeleza kielimu hivyo kuweza kuimarisha biashara yake baada ya kupata elimu itakayomfanya aendeshe biashara kifaida.
Pia Mkuu wa Idara ya Hospitali ya Wazazi Meta, Dk. John France, ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi, aliupongeza uongozi wa Chuo hicho kwa kuiona Hospitali ya Wazazi Meta na kutoa msaada wa mashuka.
Alisema msaada huo utasaidia kuboresha mazingira ya Hospitali pamoja na kuongeza ari ya utendaji kazi kwa watumishi kutokana na kufarijiwa na taasisi mbali mbali na kutoa misaada yao kutokana na kuwepo kwa hospitali nyingi zenye mahitaji tofauti lakini uongozi wa benki ukaiona Hospitali ya Wazazi ya Meta.
Aliongeza kuwa Chuo cha CBE kinatoa changamoto kwa taasisi zingine za umma kuona umuhimu wa kutembelea wagonjwa na kutoa msaada kwani jambo hilo limezoeleka kufanywa na taasisi za watu binafsi na mashirika ya dini hivyo kuzikumbusha taasisi za Serikali pia kujenga utamaduni wa kutoa misaada kwa wahitaji.
Alisema katika matibabu ya wagonjwa mbali na kutoa dawa lakini Mgonjwa hupona baadhi ya matatizo kutokana na kutembelewa na kufarijiwa ambapo alitoa wito kwa watu na taasisi zingine kuwa na utamaduni wa kuwatembelea wagonjwa na kuwafariji.
Fomu za kujiunga na Chuo hicho katika ngazi za Cheti na Diploma kwa mwaka wa masomo 2015 zimeanza kutolewa Chuoni hapo Forest ya zamani katika majengo ya Chuo Kikuu Huria jijini Mbeya.
Aidha masomo yanatarajia kuanza mwezi Machi Mwaka huu, Watu wote mnakaribishwa katika Chuo cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Mbeya.

You Might Also Like

0 comments: