Hatua za kuzifuata ili kuweza kutangaza BURE kupitia mtandao wa Karibu Mbeya
Hatua za kuzifuata ili kuweza kutangaza BURE kupitia mtandao wa Karibu MbeyaKwa mtu ambaye ni mara ya kwaza kutangaza na karibu Mbeya
1. Fungua website yetu na nenda sehemu iliyoandikwa REGISTER (www.karibumbeya.com/register/)
2. Kwenye USERNAME pale chagua jina utakalopenda kulitumia kwenye akaunti yake, unaweza ukaweka jina moja mfano Fred, au Fred John
3.Sehemu ya EMAIL hakikisha unaweka email yako ambayo inatumika au ya biashara husika kwani taarifa utakazozijaza hapo zitatumwa kwenye email.
Na pia kila utakapoisahau PASSWORD utalazimika kutumia email hiyo ili uipate ikiwa ni pamoja na kupata taarifa za mwenendo wa tangazo lako
4. Sehemu ya PASSWORD hapo utaandika neno lako la siri ingawa unashauriwa kuchanganya na namba ili kufanya isiwe rahisi kwa mtu kuweva kulijaribu na kufanikiwa kuingia kwenye akaunti yako
5. Strength indicator hii inakuoesha uimara wa neno lako la siri, kuna wakati unaandika inakuonesha neno liko WEAK kama unaliamini neno lako basi utaendelea
6. Mwisho kabisa kuna box litakucha na kukupa namba au maneno ambayo utatakiwa kuweka ili kuhakikisha kuwa wewe sio ROBOT na akaunti yako itakuwa imefunguka.
7. Ukishafungua kuna sehemu imeandikwa POST AN AD au Add New hii itakupa sasa nafasi ya kuweka tangazo lako kwa kuchagua Category yako na kisha kuweka taarifa zako za tangazo. Sehemu ya zip code na tag sio muhimu kuweka.(www.karibumbeya.com/add-new/)
0 comments: