HUWEZI KUTONGOZA? SIMU YAKO INAWEZA KUKUSAIDIA

20:33:00 Unknown 0 Comments

NAMSHUKURU Mungu kwa kunikutanisha tena nawe msomaji wangu katika busati la mashamsham. Ni siku nyingine nzuri tunapokutana mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano wa kimapenzi na leo, napenda kujadili na wewe msomaji wangu juu ya hili suala nililolitambulisha hapo juu.
Maendeleo ya teknolojia yamebadilisha mambo mengi katika maisha yetu ya kila siku. Zamani ilikuwa kama kuna mwanamke au mwanaume unampenda, basi lazima ‘umfukuzie’ kwa kumvizia vichochoroni mpaka utakapopata nafasi ya kuzungumza naye, na kama huna ujasiri wa kumtongoza ana kwa ana basi ndiyo umemkosa.
Lakini siku hizi mambo yanamalizwa kidijitali. Hata kama wewe ni ‘domo zege’, simu yako ya mkononi inaweza kukusaidia kumpata mwanamke au mwanaume wa maisha yako. Lakini je, hivi ni wote wanaojua namna ya kutumia simu kuanzisha uhusiano wa kimapenzi?
Ni matumaini yangu kuwa mada hii itakusaidia wewe ambaye muda wa kuoa umefika lakini kwa sababu moja au nyingine, huwezi kumwambia ana kwa ana mtu umpendaye. Kumbuka kuwa penzi bora ni lile ambalo wawili huanza kwa kuwa marafiki, ni makosa kukurupuka kumtongoza mtu kwenye simu bila kumvuta kwanza karibu.
Hatua ya kwanza, ukishapata namba ya simu ya huyo umpendaye, tafuta muda ambao utakuwa umetulia kisha mpigie na jitambulishe. Mweleze kwamba umempigia simu kumjulia hali, kama akikuuliza mahali ulikoipata namba yake, unaweza kumjibu vyovyote lakini inashauriwa kuwa siyo vizuri kumtajia aliyekupa namba yake kwa sababu unaweza kuwagombanisha.
Usiwe na papara, mtakie siku njema na endelea na shughuli zako nyingine. Unaweza pia kuendelea kumtumia meseji za kawaida (siyo za mapenzi), ukimjulia hali, ukimuuliza kama ameshakula au amekula chakula gani, anafanya nini kwa muda huo na vitu anavyovipenda sambamba na vile asivyovipenda.
Endelea hivyo kwa muda, siri kubwa ambayo huijui ni kwamba watu wengi, hasa wanawake huwa wanapenda kujua kuwa mtu fulani anamjali kwa kumuuliza mambo mbalimbali yanayohusu maisha yake ya kawaida.
Jitahidi kuwa mcheshi lakini usizidishe masihara. Ukishafanikiwa kumvuta karibu yako na kumfanya aamini kwamba huwa unamfikiria mara kwa mara, sasa unaweza kupiga hatua moja mbele kwa kufanya yafuatayo:
MBINU ZA KUMTEKA
Tumia sauti ya utulivu yenye hisia ndani yake, utazidi kumvuta karibu yako. Usipende kuzungumza kwa sauti ya juu au kupayuka au kupiga simu ukiwa kwenye kelele. Akipokea tu simu yako, mjulie hali yake kisha msifie kidogo kuhusu sauti yake na namna anavyozungumza.
Msimulie kidogo kuhusu siku yako inavyokwenda, tumia maneno machache lakini yatakayomfanya asiboreke kukusikiliza. Ifanye stori yako iwe ya kuvutia kwa kutumia maneno matamu yatakayomfurahisha na kumfanya aache kila anachokifanya na kukusikiliza.
Badili mazungumzo, muulize kama anajua kwamba yeye ni mzuri sana na hujawahi kukutana na mtu anayevutia kama yeye. Kama wewe ni mwanaume na unayezungumza naye ni mwanamke, utakuwa katika nafasi nzuri ya ‘kum-win’ kwa sababu wanawake wengi wanapenda sana kusifiwa.
Akiwa amekolea na sifa unazomwagia, mweleze kwamba unavutiwa naye na unatamani kuwa na mpenzi anayefanana naye. Zungumza naye kwamba atakapokubali kuwa na wewe, utamtunza na kumlea kama malkia, mweleze malengo yako ya baadaye katika uhusiano wenu endapo atakukubalia.
Usimpe nafasi ya kukwambia kama amekubali au amekataa bali hitimisha mazungumzo yenu kwa kumtakia siku njema au kazi njema. Bila shaka utamuacha akiwa na shauku kubwa ya kuendelea kusikiliza ‘mistari’ yako.
Endelea kuwasiliana naye kwa mambo ya kawaida huku ukimpima kama yale uliyomwambia anayachukuliaje. Kama naye amekupenda, utaanza kuona mabadiliko kuanzia meseji atakazokuwa anakutumia, namna anavyopokea simu yako na uchangamfu anaokuonesha.
Kama bado haoneshi dalili zozote za kukuelewa, basi jua hajavutiwa na wewe na ukiendelea kuzungumzia mambo ya mapenzi, huenda ukaanza kumboa lakini kama ana dalili za kuingia kwenye kumi na nane zako, endeleza mawasiliano naye,
omba kukutana naye sehemu tulivu kama ufukweni au popote ambapo mtakuwa wawili na hapo utakuwa na nafasi nzuri ya kueleza kwa kina juu ya hisia zako, utafikia wakati mtaelewana na kuoana.
Posted by Fred Kihwele · 1 hr · 
Mambo ya muhimu kuzingatia unapokuwa na rafiki katika maisha yako.
1. Usiwe mwepesi wa kutoa lawama na kumhukumu kwa kila jambo ila jaribu kumwelewa na kumfanya akuelewe wewe pia
2. Usijifanye kuwa wewe ni wa muhimu kuliko yeye ila amini yeye ni wa muhimu zaidi jambo litakalo mfundisha nae kukuona wa muhimu
...See More
Like ·  ·  · 613
Posted by Fred Kihwele · 1 hr · 
Je unahitaji samani bora na za kisasa kwa bei nafuu?
Tembelea www.karibumbeya.com na ukutane na duka lenye samani bora kwako
Tunatengeneza Sofa set mpya na Ku Repair sofa set za zamani iwe ni Kitambaa,ngozi au leather na pia tunachange Muundo wa Masofa yako Toka Moja kwenda mwingine T...
KARIBUMBEYA.COM
Like ·  ·  · 3
Naona wadau wengi wana matatizo ya software ya huawei hivyo basi nimeona nishare na watu idea kadhaa za kusolve hizi problems.
Kwanza itabidi udownload correct firmware ya model yako kisha extract utakuta file la dload weka kwenye sd-card.
Ukimaliza power off your phone kisha shikilia volume up + volume down + power button kisha itaanza kuupdate.
Hii ndo first line way ya kusolve matatizo ya huawei kama itatokea pink screen ujue ujaweka vizuri file la dload kunazingine huawei...
See More
Like ·  ·  · 3
Una fikiria kufanya nini weekkend hii

ww.karibumbeya.com inakurahisishia ratiba yako kwa kukuwekea kiganjani mwako list ya vile uvitakavyo kwa weekend hii.
Karibu mbeya is a leading mbeya’s online site which provides you an opportunity to get several goods and services being available here in Mbeya and other neighboring places. Read more
KARIBUMBEYA.COM

You Might Also Like

0 comments: