DAKTARI AGOMEA KUITOA MIMBA KISAAA:........:.

08:49:00 Unknown 0 Comments



Mama mmoja alienda kwa daktari akiwa na hofu na kumwomba daktari ampe msaada wa haraka kwani alikuwa amechanganyikiwa na hajui nini afanye.

Mama akamwambia daktari nina mimba na mtoto huyu niliyenaye hapa bado ni mdogo na nahofia kwani siwezi kuwa na mtoto mwingine mdogo wakati huyu bado hajakua.

Daktari akatabasamu kwa muda na kisha akamwambia mama nafikiri nimepata njia rahisi ya kukusaidia ambayo itakuwa ya afadhali zaidi.

Mama akafurahi kuona daktari kapata jibu na kumwambia ya kuwa asante daktari naomba uniambie nitafanyaje.

Daktari akasema, sasa mama nafikiri iliniweze kukusaidia uwe na mtoto mmoja ngoja tumuue huyu ambaye unaye hapa na aliye tumboni akue na kisha ujifungue na kumtunza.

Mama kwa mshangao akasema wewe daktari acha kabisa maneno yako huoni kama huo ni uuaji tena wa makusudi kabisa????? hapana siwezi kabisa.

Dakatri akasema, kwa kuwa lengo lako ni kuwa na mtoto mmoja sikuona utofauti kati ya kumuua aliye tumboni na huyu ambaye mzima kwani vyote ni uuaji.

Mama yule akaanza kulia kwa uchungu na kukataa kutoa mimba na daktari akafurahi kwa kuwa ameweza kuokoa maisha ya mtoto aliye tumboni.

Comment "Mbaya sana kutoa mimba" kisha share kama unachukizwa na vitendo hivyo

kisha like Tabasamu na Fuledi

You Might Also Like

0 comments: