Soma jinsi shina la mboga ya ajabu lilivyoishangaza famlia fulani

07:57:00 Unknown 0 Comments



Kuna familia moja ambayo baba alifariki na mama kuwa na jukumu la kuilea familia yenye watoto wanne kwa shida sana.

Mama huyu pia alikuwa akikaa na watoto wawili ambao aliwachukua awatunze baada ya mama na baba yao kufa katika ajali mbaya ya basi mika michache kabla ya yeye pia kufiwa na mme wake.

Maisha hayakuwa marahisi kwani mama alihitajika kuamka asubuhi na mapema na kwenda sokoni kufanya biashara ili aweze kupata fedha ya kumwezesha kuyakidhi vyema mahitaji ya familia yake.

Siku moja mama huyu alizunguka nyuma ya nyumba yake akiwa anafanya usafi na kuona kuna mashina matano ya mboga aina ya figiri na yakiwa yamestawi sana.

Akashangazwa na alichokiona na kuamua kuchuma mboga zote zile na kuzipaki vizuri ili aende akauze sokoni na chache kuweka kwa ajili ya chakula cha yeye na familia yake.

Maajabu ya mashina  yale ya mbona ni kwamba kila alipoyachuma siku mbili baadae alishuhudia mboga zikiwa zimechanua zaidi na kuzichuma kwenda kuuza tena.

Hatimaye yale mashina yakawa yakitoa mboga nyingi kwa wiki na kumwingizia fedha nyingi na kwa huruma ya mama akawa akiwapa majirani zake pia.

Hakuwa na roho mbaya zaidi ya kuwaaambia wachume na kwenda kula na familia zao  baada ya yeye kuchuma za kuuza kwani aliona kwake ni kama muujiza wa baraka kutoka kwa Mungu hivyo ilikuwa ni busara kugawana na majirani zake hao.

Watoto wake hawakupenda ile tabia ya mama yao ya kuwapatia majirani zao zile mboga kwa kuwa hapo mwanzo wale majirani waliwanyanyasa kwa kuwalipisha bei kubwa kwenye maji yao au hata kutowapa kabisa.

Mama aliwasihi watoto wake kuwa kila mara usihesabu makosa ya wenzako na kuwawekea kinyongo au hata kuwahukumu kwani Mungu wetu ni wa upendo na anapenda tupendane na kugawana baraka alizotujalia kwa furaha.

Miezi michache baadae yule mama alifariki kwa ajali ya basi na walipotoka msibani hawakakukaa muda mrefu yale mashina ya mboga yakanyauka na hawakujua kwa nini.

Baada ya kukaa na kuulizana wakagungua kuna mmoja wao alikuwa akiwakatalia majirani wale kila walipotaka kuchuma mboga zile kwa kuwafungia geti.

Hivyo hio ukawa mwishi wa mboga zile na wao sasa wakaanza kununua mbali tena kwa bei kubwa zaidi jambo ambalo mwanzoni halikuwa kwenye bajeti yao.

Rafiki wa fuledi, kila ulichojaliwa kukipata kwa bahati jaribu kukutumia kwa uangali na upendo wa dhati huku ukimshukuru Mungu kwa upendeleo huo na kugawana na wale wenye shida na Mungu wetu atakuongezea mara mia zaidi ya ulichokitoa.

Hebu ona mfano wa huyu mama ambaye yeye aliishi kwa furaha na kuwasaidia wenzake na akabarikiwa kwa kuletewa mashina ya mboga kimaajabu.

N mashina haya  yakamwingizia hela nyingi lakini bado hakuwa na roho mbaya ya kuwanyima majirani zake wenye shida kaka yeye hata kama mwanzoni walimnyanyasa na maji yao.

Kifo cha yule mama kikaondoka na baraka zote jambo linalonifanya nikumbuke kuwa kuna wakati unaweza ona umebarikiwa na kujisifu kumbe watembelea nyota ya mwenzio. 

Mfano mzuri ni kupitia watoto wa mama huyu walivyoona ni haki yao kuwa na mashina yale na kuwanyima majirani na mama alipoondoka nayo yakanyauka.

Hebu jiulize ni mara ngapi unakuwa na rafiki ambaye kila mfanyalo lafanikiwa na mkiachana unaona kuna vitu haviko sawa tofauti na mwanzo???

 Au umewahi kuwa na mtu akatika familia alifanikiwa na baadae akaja tena kuwa maskini... jiulize wapi alikosea zaidi ya kuwa na roho mbaya???

Au mwingine alikuwa na mafanikio na baada ya kufa mali zake zinapotea baada ya familia kushindwa kuelewana????

Je wewe ni mara ngapi unaona ufahari kutumia gari lako au chochote ulichonacho na kuwanyanyasa wenzako?

***Kumbuka mafanikio hayaji kwa kuwa na roho mbaya na pia Mungu huwabariki wale ambao hushukuru kila baraka maishani mwao na kuwa na upendo kwa wenzao***

Sala yangu kwako... "Baba Mungu namwombea kijana anayeusoma ujumbe huu umpe hekima na busara ya kutumia vyema baraka ulizomjalia huku akiwakumbuka na wenzake wenye uhitaji. 

Na kwa kila roho nzuri atakayoionyesha kwa wenzake naomba umjalie furaha na mafanikio mara kumi yake.

Mwondolee roho mbaya ya kuwachukia wenzake au wivu usio wa mafanikio bali mpe mafanikio kila siku ..AMEN"


USIUDHARAU UJUMBE HUU

You Might Also Like

0 comments: