MSONGO WA MAWAZO NA VIFO VYAKE KAA CHONJO.

07:54:00 Unknown 0 Comments




MSONGO WA MAWAZO NA VIFO VYAKE KAA CHONJO.

Ni vyema kwa mara nyingine nikiongelea ugonjwa huu wa usongo wa mawazo ili rafiki zangu wanaonifuatilia katika mada zangu waweze kuchukuwa tahadhari kwani ni ugonjwa kama magonjwa mengine ya hatari. Asili ya ugonjwa huu ni stress, wasiwasi, ulevi wa pombe kali, madawa ya kulevya na mara nyingi pia hutokana na kutumia dawa fulani unazotumia kwa kutibu ugonjwa mwingine kwa mfano dawa nyingi za VVU zina side effect ya usongo wa mawazo.

Ugonjwa huu wa msongo wa mawazo kwa jina lingine unaitwa depression, dawa za kutibu msongo wa mawazo zipo, kwa mfano zoloft 20mg, elavil 25 mg mara nyingi huanza kufanya kazi yake siku tano hadi wiki mbili, na ukae ukijuwa kuwa kadri unavyotumia dawa hizi pia huzaa side effect, au kuongeza ugonjwa mwingine kutokana na matumizi ya dawa hizi, ama kwa hakika kama zilivyo dawa zingne unatakiwa uzitumie kila siku kulingana na maelekezo ya dakitari wako, kama umeanza kuzitumia na ukaziacha ghafla utapata ugonjwa mwingine unaitwa withdrawal, kuziacha dawa hizi inabidi uziache kwa mpango wa taratibu. Pia matibabu mengine ni mafunzo nasaha kutoka kwa wataalam wa magonjwa ya psych.

Utamjuaje mgonjwa wa msongo wa mawazo, anapenda kunywa pombe sana,kuvuta sigara sana, mpweke, anajitenga na wenzake (kukaa pekee yake), uzito wake kupunguwa, kujiongelesha mwenyewe, kuwa na hasira, kuongea vitu visivyowezekana, kuishiwa hamu ya kufanya tendo la ndoa, na pia kujiuwa. mara nyingi mgonjwa wa usongo wa mawazo hujiuwa wakati unamwona amepona, na dalili moja wapo ya tahadhali kuona kama mgonjwa huyu anataka kujiuwa ni kuanza kugawa vitu vyake kwa watu bure, kwa mfano saa, gari, mashamba, pesa na vitu vingine vyovyote anavyomiliki, ukiona dalili hii ni vyema ukampeleka hospitali mapema na kuwa naye muda wote (one-o-one)

Kujiepusha na ugonjwa huu ni kupunguza stress, kuridhika na hali halisi uliyo nayo, usifikirie sana juu ya maisha yako, kuwa mtu wa mskitini au kanisani, jihusihe katika hadhara ya watu, usinywe pombe kupita kiasi, usitumie dawa za kulevya na pia jiepushe kukasirika. Kama utakuwa na maswali au kuongezea unakaribishwa.

You Might Also Like

0 comments: