LAKINI HIVI NI KWELI WANAWAKE WENGI HATUPENDANI???? Au tunasingiziwa?

'.....Wanawake hampendani nyie....' nikaambiwa hivi na mie nikamtolea macho kwelikweli nikiuliza kwasababu zipi za msingi?
Akaanza
1. Wenzenu wawili wamechukua fomu za urais....nilitarajia mlipuko flani wa pongezi kwa uthubutu hata kama si sapoti ya kura ila hollaaa.... (nikatulia tu)
1. Wenzenu wawili wamechukua fomu za urais....nilitarajia mlipuko flani wa pongezi kwa uthubutu hata kama si sapoti ya kura ila hollaaa.... (nikatulia tu)
2. Wanaoongoza kutukanana na kuumbuana mitandaoni ni wanawake... uongo? (nikatulia tuuu)
3. Wewe si una blog? nikajibu ndio... akaniambia kuna mwanamke mwenzio unayemuita rafiki ameshawahi kukusapoti kwa kukutangazia blog yako kwenye wall yake? nikatoa macho ndiii
4. Angalia manesi na wajawazito...
etc etc etc
5. Nataka ujue ukiona neno women supporting women ujue ni anayesapoti alishasapotiwa anarudisha shukrani tu.... vinginevyo mwanamke kumsapoti mwenzake akijua wazi sapoti anayompa haimfaidishi yeye kwa lolote hutokea mara chache saaaaaana....
Nikacheeeeka! Nikamwambia ya wanawake tuachie wanawake.... tunajuana wenyewe....
LAKINI HIVI NI KWELI WANAWAKE WENGI HATUPENDANI???? Au tunasingiziwa?

0 comments: