Maisha ya mjini ya shida zake hasa kwa mama ambaye pia ni mfanyakazi.

16:36:00 Unknown 0 Comments

Maisha ya mjini ya shida zake hasa kwa mama ambaye pia ni mfanyakazi.
Nasema hivyo kwani ili uweze kutimiza na majukumu mengine ya kifamilia huna jinsi zaidi ya kumtafuta masaidizi wa majukumu nyumbani kwako.
Ni wakati huu ambapo nilihitaji kumtafuta msichana wa kazi ili anisaidie hasa kuwa na watoto niwapo kazini.
Nilibahatika kumpata binti mmoja kutoka kijijini kwetu na akaanza kuwa msaada pale nyumbani na siku zikaanza kusonga mbele.
Kuna mambo nikagundua yakianza kubadilika siku zilivyozidi kwenda pale nyumbani.
Kwanza wanangu walianza kuwa na kiburi, mimi na mme wangu ugomvi kila siku na kama haitoshi nyumba ikaanza kuwa kama uwanja wa vita usioisha kelele na hakuna tena amani na furaha.
Hali hii ikaanza kunipa wasiwasi kwani sikutambua nini kimesababisha hali hiyo au nani yuko nyuma ya hali hii.
Mara mme wangu kwenye biashara zake zikaanza kwenda mrama na wakati nikiwa katika tafakari hizo mme wangu akapata ajali mbaya na kumfanya avunjike mguu.
Nikawa namuuguza nyumbani na hata kabla hajapona mtoto wangu akamwagikiwa na maji ya moto nikiwa kazini na kunifanya kuwa na wagonjwa wawili pale nyumbani.
Hali ikazidi kuwa ngumu huku nikiwa sijui ni nini kinaandama familia yangu.
Huwezi amani kila nilivyolotatua hili mara jipya nikaibuka na sasa tukaanza kuunyemelea umaskini kwani hakuna kitu tulichokifanya kikafanikiwa.
Mambo yakazidi kuwa mambo kwani wakati huo nilikuwa na mimba ya miezi minne na siku kadhaa ikatoka kimiujiza nasema hivyo kwani hata sikuwa na dalili yoyote ya kuumwa wala nini lakini ikatoka nikafikiri labda ni msongo wa mawazo ya hali yetu.
Nililazwa kwa siku kadhaa na kuruhusiwa na nilipofika tu nyumbani hali yangu ilibadilika na kurudishwa tena hospitali.
Hapa nikaona sina jinsi na kuomba niitiwe mchungaji kwani niliona mauti yakiniandama. Alikuja mchungaji na kuniombea na baada ya wiki nilirudi nyumbani baada ya kuruhusiwa.
Nikamwalika mchungaji kwa ajili ya kuiombea familia yetu. Siwezi kuamini kuwa binti wa kazi ndio alikuwa nyuma matatizo hayo yote.
" nilitumwa kuwa kila familia itakayo kaa na mimi ni lazima ikose furaha na kuanguka kwa kila mipango yao na kuwapa matatizo" yalikuwa ni maneno ya huyi binti baada ya kuhojiwa na mchunguji wakati wa maombi.
Nilimrudisha binti huyo kwao na namshukuru Mungu kwa kuniokoa na mambo makubwa ambayo yangeweza kuja kutokea kwa kuendelea kukaa na yule binti bila kujua.
Hivi sasa familia imerudi na kuwa na amani na furaha na mme wangu kapona na kazi zake zinaendelea vyema.
"Naogopa kabisa kuwa na binti wa kazi" alimaliza kusimulia kisa hiki cha kutunga mama huyo aitwaye mama pachu na kwenda kanisani

You Might Also Like

0 comments: