Nimezipenda hizi tips embu na wewe zikusaidie!! UMEWAHI ONA HII...
chumvi ikizidi kwenye wali weka kiazi mviringo katikati kikiwa kimemenywa chumvi itapungua.
kama choo chako, kina harufu, ya mkojo na huna dawa washa kiberiti chooni harufu itakwisha
chukua ganda la limao lichome na vipisi vya karafuu weka kila pembe ya chumba mbu utawasikia kwa jirani
kutoa harufu kwenye wali uliongua weka kipande cha mkaa harufu ya kuungua itakata
km umepika mchuzi upo maji maji yaani mwepesi labda maji yamezidi chukua kiazi kikune na cha kukunia nyanya weka chuzi litakuwa rost
kuivisha maharage faster chukua maji yalochemka tia maharage weka kwenye chupa ya chai funga kesho mimina kwenye sufuria pika nusu saa harage litakuwa lishaiva
ukipika mchuzi vitunguu vikiungua weka sukari kidogo harufu ya kuungua haitasikika
Ukiamaliza kuosha vyombo still wire iweke kweny maji haiharibiki utaendelea kutumia kesho
big g ikiganda kwenye nguo weka kweny friza ikiganda itatoka kirahisi
kuondoa harufu ya uvundo kwenye fridge weka baking soda kwenye kikombe na maji kidogo weka kwenye fridge...

Waaaah
ReplyDelete