Tabasamu na Fuledi yanisababishia majanga
Baada ya takribani miaka 2 hatimaye ijumaa ya jana nilishawishiwa kutoka na kwenda kiwanja kujirusha. Kwa zaidi ya miaka 2 mimi na kujirusha hatujawa beneti kihivyo. Lakini wikiendi jana nilivunja huo mwiko.
Basi bana sisteri mmoja tuliyefahamiana hapa Tabasamu na Fuledi akanipigia simu ile Jana jioni akinitaka tukutane Babs Longe club (sijui ndio inavyoitwa hivyo...wenye kujua saidieni). Nikasita kidogo kwani kama nilivyosema mimi kujirusha sio zangu kabisa. Lakini kwa ajili yake nikakubali.
Nikajipiga sopusopu na baada ya hapo nikaingia kwenye mchuma huyo nikaenda kumpitia. Nikamkuta naye kajikwatua kwelikweli...naona hakutaka mchezo kabisa. Akaingia kwenye mkebe nami nikapiga moto chini. Nadhani allipenda cologne niliyokuwa nimepakaa maana usiku mzima hakuacha kunipa compliments....'mmm jamani Ngadu unanukia vizuri...umepakaa nini?'....'Aaah nimepakaa Cartier Roadster Sport exclusive kutoka Nieman Marcus'....akasema kwa mshangao 'wee Ngadu sikuwezi...yaani hata cologne unanunulia Nieman Marcus!!'
Kuifupisha hadithi ndefu, tukaingia zetu hapo Club. Tukajirusha....vinywaji vya hapa na pale...yeye ni mpenzi wa Long Savana na mimi mtu wa bia tu.
Basi tukafurahia usiku wetu halafu tukaondoka. Alikuwa kachoka na hakutaka nimrudishe kwake. Basi tukaenda wote kwangu.
Tukafika nyumbani tukaenda moja kwa moja chumbani.
Tukachojoa mavazi tukapanda kitandani. Mara mwenzangu akaniambia anasikia baridi....mwanamume nikajua leo hapa kitu na boksi. Basi nikaanza kumtomasa tomasa hapo na jambo moja likapelekea jambo jingine na hatimaye nikajikuta niko juu ya kiuno chake na kilichofuatia baada ya hapo tumia imagination yako.
Shughuli ikawa ndio imeanza kukolea sasa. Mazee nilikuwa nagusa engo zote...kaskazini, kusini, mangharibi (sio magharibi), mashariki, kaskazini mangharibi, kusini mashariki...yaaani wewe acha tu.Mototo alikuwa bomba na mtamu balaa, yaani hadi raha.
Sasa wakati karibia nafikia kilele mara kawa ananikiss sikioni kwa mbwembwe za kila aina mara ghafla bin vuuu nikaamka toka usingizini bana. Baada ya kutahamaki nikagundua kumbe nilikuwa ndotoni na mbwa wangu alikuwa akinilamba mikono maana sikunawa baaada ya kula na nililala sebuleni bana....aisee niliudhika sana na nikabakia kufyonya na kutukana. Yaani yale maraha yote kumbe nilikuwa naota bana...aaah basi hata kulala sikuweza tena. Ikabidi niamke tu nianze kuangalia tivii na kusoma Tabasamu na Fuledi.
Hiyo ndio ilikuwa ndoto yangu ya usiku wa ijumaa kuamkia jumamosi.
Ngoja niendelee kuamini nitapata mrembo kupitia Tabasamu na Fuledi.

0 comments: