Cha fasta

15:39:00 Unknown 0 Comments






Dada mmoja aliibiwa mkoba wake ambao ndani yake kulikuwa na simu, kadi ya benki, wallet yenye hela pamoja na info zake kibao.

Dada yule kwa kuwa aliibiwa akiwa anaangia kwenye daladala  na baada ya kutumia muda mrefu akiwa kwenye foleni baada ya kufika kituoni ikamdidi akimbie kwenye kibanda cha simu na kumpigia mme wake kumwambia ameibiwa kila kitu.

Mme  wake akamwambia mbona nilipokea ujumbe muda kidogo ukinitaka nikupe namba za siri za mpesa, tigopesa na ile ya benki nami nishatuma.

Jamaa na mkewe wakakutana na kukimbia benki fasta kufika pale wakakutana na majanga, hela zote zishazolewa benki,na mpesa na tigo pesa zote ziko nyeupe na kitendo hicho kimefanyika ndani ya muda mfupi tangu dada aibiwe.

Funzo

1. Kwenye simu usipende kuonyesha majina ya watu muhimu sana kama vile nyumbani,Mpenzi,mume, Darl, Honey, Hubby, Sweetheart, Dad, Mom na mengineyo...

{Ila andika mfano majina mfano  cha fasta, zee jinga, mpuuzi nk}

2. Nivizuri ukipata ujumbe kabla ya kujibu mpigie mtu kwanza hasa kama anaomba mambo ya  muhimu kama hayo

{Ila sijasema usimpe mpezi wako namba za siri au kama huna ndiouanze kudai sasa .. hapana}

3. Kuwa makini unapotembea ukiwa na vitu vya muhimu kama hivyo

You Might Also Like

0 comments: