Fursa ya kujitambua hii hapa

19:11:00 Unknown 0 Comments





"KUJITAMBUA"

Siku moja NDEGE alimuuliza swali NYUKI hasa baada ya kumwona anavyojituma huku na huko ili atengeneze asali.

NDEGE, "Hivi haumii kuona unatengeneza asali kwa kutumia nguvu kubwa ... lakini binadamu anakuibia kila siku, Je haujisikii vibaya?"

NYUKI, akamjibu NDEGE kuwa, "Kamwe siwezi kumia wala kuogopa"

Kwa sababu binadamu ataniibia asali tu, ila kamwe hataweza kuiba uwezo wangu au ujuzi wa kuiandaa asali hii.

Funzo

Watu watakuumiza kwa kukuibia mawazo yako uliyowashirikisha lakini kumbuka hakuna atakayekuibia uwezo wa kuweka wazo jingine mezani.

Kazana kuwa mbunifu mwenye kutokata tamaa na pia tambua uwezo wako ulipo sasa

You Might Also Like

0 comments: