MUNGU ANAWAONA ACHENI HIZO MAMBO

15:02:00 Unknown 0 Comments

Story inaanza hivi.....

Pichani mtoto huyu na wadogo zake maisha yao yalikuwa ni ya raha sana wakati wazazi wao walipokuwa hai, Baba mfanya biashara na Mama Mwalimu...

Matatizo yalianza pale wazazi wote walipofariki katika ajali ya gari iliyotokea Mbeya ambapo gari ilitumbukia katika mlima nyoka na wazazi wake kufariki pamoja na wadogo zake wawili na kubaki yeye na dada yake wa kwanza ambaye nae alikuwa kidato cha pili..

Baada ya hapo, mali za marehemu baba yake zilitaifishwa na Benki kwani baba yake alikopa Benk na nyingine marafiki wa baba katika biashara kugombania hivyo kuwachia nguo tu na mali kidogo ambazo ndugu wa baba yake walizigawana.

Mirathi ya mama yao ilitoka lakini shangazi zake walidai kuwa madogo hawana chao, hivyo wakaachwa juu juu na wao wakaamua kwenda dar kusaka maisha.

Dada yeye akawa house girl na dogo akawa akizunguka mtaani kusaka riziki.

Kwa sasa dogo anataabika hana pa kulala wala kula na hana msaada wowote na dada yake kashanyiwa mikasa ya ajabu na sasa hajulikani alipo..

Nyie ndugu msio na roho za huruma acheni tabia hizo kwani Mungu anaona mnayoyafanya...!!


Mkiwa makanisani mnajifanya kutoa sana sadaka kumcha Mungu lakini nyuma yenu mnafanya mambo ya ajabu ya kugombania mali za marehemu na kuwacha vijana wanasota mtaani bila huruma na wakati wazazi wapo mlijifanya kina anko safi


You Might Also Like

0 comments: