Na kifo kikamkwepa kiutani utani yaani

16:36:00 Unknown 0 Comments


Fuledi alikuwa anatoka kijiji A kwenda kijiji B majira ya usiku, ghafla alipatwa na pancha katika tairi lake la mbele na ikambidi asimame kwa ajili ya matengenezo.

Akiwa anaendelea kulitengeneza gari lake katika mbuga zile mara akaona viumbe vya ajabu ajabu vikimsogelea. Akakaza macho na kuzidi kutazama ili apate picha yao vizuri bado akaona kuwa uhai ulikuwa ukingoni kabisa.
Kwa kuwa alijua kuwa ni lazima afe kwani viumbe wale walikuwa wa hatari na wenye uchu wa kumtoa roho, yeye alifikiri kwa sekunde chache na kisha akasema moyoni maneno haya, “Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. Kisha akafumba macho yake, na kusema “ Mungu naenda kufa leo, hivyo naomba unipumzishe kwa amani”

Baada ya kufumbua macho yake, wale viumbe walikuwa wameshapotea na kwa mbali kulikuwa na mwanga wa gari lililopita pale na kumpamsaada na kuondoka zake.

Mtegemee MUNGU katika matatizo yako yote


You Might Also Like

0 comments: